23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAUZO SOKO LA HISA YAPOROMOKA

Na JOHANES RESPICHIUS -DAR ES SALAAM


HALI ya mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam imeendelea kuwa mbaya baada wiki hii kushuka kwa asilimia 37 kutoka Sh bilioni 6.4 hadi kufikia Sh bilioni 4 ambapo wiki iliyopita yalishuka kwa asilimia 23.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa DSE, Patrick Mususa, alisema licha ya idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kupanda mara sita wiki iliyopita, wiki hii zimeshuka kwa asilimia 94 hadi laki 6.71 kutoka milioni 11.1 wiki iliyopita.

mtz11

“Benki ya CRDB imeendelea kuongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa asilimia 42.40 licha ya wiki iliyopita kuongoza kwa asilimia 95.45 ikifuatiwa na Kampuni ya Bia, TBL kwa asilimia 41.44 kutoka asilimia 2.18 na DSE kwa asilimia 6.44 kutoka 1.44 wiki iliyopita.

“Pia ukubwa wa mtaji wa soko nao umeendelea kushuka ambapo wiki hii umeshuka kwa asilimia 2.4 na kufika Sh trilioni 20.9 kutoka Sh trilioni 21.4 wiki iliyopita baada ya wiki hiyo kushuka kwa asilimia 2.1.

“Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani pia umeshuka kwa wastani wa asilimia 0.6 hadi trilioni 8.14 kutoka trilioni 8.19 ukilinganisha na wiki iliyopita kushuka kwa asilimia 0.3,” alisema Mususa.

Kwa upande wa viashiria vya soko, Mususa alisema kiashiria cha sekta ya viwanda kimejitokeza kupungua kwa pointi 40.84 baada ya bei ya hisa za TCCL na TBL kupungua kwa asilimia 13.98 na 0.74.

Aidha alisema viashiria vya sekta ya huduma za kibenki na kifedha wiki hii ilibaki kwenye wastani ule ule wa Sh 2,771.18 na sekta ya huduma za kibiashara kwenye wastani wa Sh 3,157.95.

Akizungumzia sababu za kushuka kwa idadi hiyo ya mauzo ya hisa, Mususa alisema imechangiwa na wanahisa wenyewe ambapo wiki nyingine hujitokeza kuuza hisa zao na mara nyingine hukataa kuuza.

“Kushuka au kupanda kwa mauzo kunategemeana na utashi wa wanahisa wenyewe kutaka kuuza hisa zao ambapo kuna wiki ambazo huuza hisa nyingi na nyingine kuuza chache hivyo hivyo bei nayo hupanda na kushuka,” alisema Mususa.

Hata hivyo, alisema soko hilo la hisa hapa nchini (DSE) linaendelea katika kiwango kizuri cha mauzo ikilinganishwa na nchi za Afrika Mashariki likiwa nyuma ya soko la hisa la Nairobi (NSE) na kwamba NSE inaonekana kufanya vizuri kwa sababu ina kampuni nyingi zaidi ya DSE.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles