26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Maurice: Urasimu ni kikwazo kwa wawekezaji wazawa

0D6A8334NA FARAJA MASINDE, DAR ES SALAAM

TANZANIA ni nchi iliyobarikiwa kuwa na maeneo mazuri ambayo ni rafiki kwa kufanya kila aina ya uwekezaji, kwa kuliona hilo wadau mbalimbali hususan wapenda maendeleo wamekuwa mstari wa mbele kutaka kutumia fursa hiyo kwa kuifanya iwe sehemu yenye ustawi mzuri na mazingira safi ya kuishi.

Lakini hayo yote yamekuwa si kitu rahisi kwa wawekezaji wazalendo kupata nafasi ya kufanya maendeleo ikilinganishwa na ile nafasi wanayoipata wawekezaje kutoka nje ya Tanzania, ambao wamerahisishiwa mno na kufunguliwa milango ya kuwekeza kwenye ardhi yetu.

Kuwapo kwa urasimu huo, ndiko kunakofanya wawekezaji wengi wazalendo kushindwa kutimiza mipango yao licha ya kuwa na manufaa makubwa kwa Taifa, kwa kuwa imekuwa ni kawaida kuona wawekezaji hawa wakishindwa kupewa kipaumbele kwenye nchi yao wenyewe ikilinganishwa na wageni ambao kwao imekuwa ni rahisi.

Johnson Maurice, ni kati ya wawekezaji wazawa ambao wamekumbana na changamoto hiyo ya kushindwa kuungwa mkono na serikali licha ya kuwa na mkakati mzuri unaolenga kutoa fursa lukuki kwa Watanzania.

Maurice kupitia Kampuni ya Maurice and Five Brothers Enterprises, ambayo yeye ni Mkurugenzi wake, tayari amekuwa na mkakati wa kuanzisha mradi mkubwa ambao utakuwa na huduma zote muhimu, ambao anaamini iwapo utafanikiwa basi si tu utafanya madhari ya Jiji la Dar es Salaam yaendelee kuwa ya kisasa bali pia utakuwa umeinua uchumi wan chi kwa kiwango kikubwa.

Maurice anasema ili kuthibitisha kuwa anadhamira ya dhati y kuleta maendeleo nchini, ametenga eneo kwa ajili ya mradi huo lililoko Mbande Kisewe, Mbagala jijini Dar es Salaam.

“Lengo ni kufanya Manispaa ya Temeke kuwa na madhari ya kisaasa, mradi huu utahusisha uwepo wa kituo cha mabasi makubwa yaendayo nje na ndani ya nchi, pia kutakuwa na sehemu kwa ajili ya maduka makubwa na ya kisasa ‘Shopping Mall’ hali ambayo itapunguza msongamano mkubwa wa watu kwenda mjini,” anasema Maurice.

Anasema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza adha kwa wakazi wengi wa maendeo hayo kulazimika kwenda kupanda gari katika Kituo cha Mabasi ya Mikoani Ubungo na badala yake itakuwa ni rahisi kwao kupata huduma hizo za usafiri kwenye kituo hicho kitakacho jengwa ndani ya mradi huo.

Katika kulifanikisha hilo, alishawasilisha mpango wake huo katika Manispaa ya Temeke.

“Manispaa hiyo ndiyo yenye mamlaka ya kuendesha mradi huo hivyo, niliwapelekea mradi wangu kwa ajili ya kuona kuwa ni kwa namna gani tungeweza kufanikisha mpango huu, walipitia mpango kazi huo na kuona kwamba ni jambo jema na kunipongeza kwa kuwa na mkakati mzuri wa kubuni mradi wenye faida.

“Lakini juhudi za manispaa kushikamana na mimi katika kufanikisha mradi huu ziligonga mwamba kutokana na kutokuwa na fedha, badala yake ikaniandikia barua Machi 25, mwaka jana, ya kunitaka nijaribu kutafuta ubia kwa watu wengine kwa kuwa wao wanakabiliwa na tatizo la ukusanyaji mdogo wa mapato, pia wanakabiliwa na madeni mengi,” anasema Maurice.

Barua hiyo ilikuwa ikisema; “Baada ya majadiliano ya kina katika kikao kilichofanyika januari 16 mwaka jana, tulikubaliana wataalamu wa halmashauri wafanye upembuzi yakinifu wa awali kupima manufaa ya mradi kiuchumi na kijamii.

“Upembuzi yakinifu umeonesha huu mradi utakuwa na manufaa makubwa kiuchumi na kijamii katika eneo hilo. Kutokana na hali halisi ya ufinyu wa bajeti ukilinganisha na majukumu iliyonayo, halmashauri haitaweza kuingia ubia/kuwa na hisa katika mradi huu.

“Kwa barua hii tunapenda kukueleza kukuarifu kwamba unaweza kuendelea kutekeleza mradi huu pasipo ubia na halmashauri, kwa kuzingatia sheria na miongozo ya serikali katika kutekeleza miradi ya aiana hii. Halmashauri itakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa masuala mbalimbali yaliyo chini ya mamalaka yake,” ilisema sehemu ya barua hiyo iliyoandikwa na kaimu mkurugenzi.

Maurice anabainisha kuwa manispaa hiyo ilimpa barua ambayo ina baraka zote kwa ajili ya kupata mbia wa kushirikiana kukamilisha mradi huo, ambao anasema mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha Sh bilioni 10 mpaka 15 fedha ambayo yeye binafsi ingekuwa si rahisi kuwa nayo.

Anasema mara baada ya kubaini kiasi hicho cha fedha ambacho kwa Mtanzania wa kawaida kuwa nacho ni kitendawili, aliamua kufanya mawasilianano na Balozi wa Tanzania nchini China, Abdulrahman Shimbo.

“Kwa bahati nzuri balozi huyo aliniunganisha na kampuni moja ambayo inatenda ya kujenga kituo kipya cha mabasi cha Ubungo hivyo, wangeweza kuunganisha mradi huo kwa pamoja japo kulikuwa na ugumu kutokana na kampuni hiyo kutokuwa tayari kuja nchini kwa wakati huo,” anasema Maurice.

Baada ya kushindikana kwenye kampuni hiyo ya kigeni, aliamua kwenda Mfuko wa Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambao ndio wanaoshughulikia masuala yote ya biashara kwa sekta binafsi, ambapo waliweza kuupitia mradi huo na kubaini kuwa na manufaa.

“Walikubaliana na mradi wangu huo na kufikia uamuzi wa kumshirikisha mwekezaji wa nje ya nchi, ambapo tuliwafuata Umoja wa Ulaya, ambao walileta mwakilishi wao kuja kuangalia mradi huo na kusema kwamba ni mradi mzuri lakini umekosewa katika kuuandaa.

“Kutoakana na changamito hiyo umoja huo ulishauri kusukwa upya jambo ambalo lilikuwa linagharimu kiasi kikubwa cha fedha, lakini hata hivyo juhudi hizo hazikuzaa matunda kutokana na Umoja wa Ulaya kutaka kumalizika kwa kipindi cha uchaguzi,” anasema.

Anasema lengo lake ni kuona mradi huo ambao umejaa tija lukuki ukifanikiwa licha ya ukweli kuwa bado hajapata pa kuanzia kutokana na kukosa fedha.

Anasema kuwa imekuwa ni kazi kubwa kupata mkopo za kufanikisha mradi huo kwa sababu ya masharti magumu yanayotolewa na benki nyingi nchini.

“Sote tunatambua kuwa katika kikao ambacho alifanya rais aliyeko madarakani na wafanyabiashara, alisema ni wakati sasa kwa wawekezaji wa ndani kupewa kipaumbele katika kukamilisha mikakati yao na kuahidi pindi mtu anapokuwa na changamoto yoyote basi milango iko wazi serikalini.

“Lakini utabaini kuwa bado kuna changamoto nyingi ambazo zinafanya mambo kuwa magumu hasa kwa wawekezaji wazawa ikilinganishwa na wageni.

“Hivyo ni wakati sasa wa serikali sambamba na mifuko mbalimbali ya hifadhi za jamii na ule wa Dhamana ya Uwekwezaji (UTT), kuona ni kwa namna gani tutakavyoweza kushirikiana katika kuhakikisha kuwa mradi huu unafanikiwa.

“Milango iko wazi kwa yeyote atakayekuwa tayari kushirikiana nami katika kukamilisha mradi huu, ili kuifanya Tanzania hususan Jiji la Dar es Salaam kuwa la kisasa zaidi,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles