Imechapishwa: Wed, Sep 13th, 2017

MATTAKA WA ATCL JELA MIAKA SITA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Elisaph Ikomba wamehukumiwa jela miaka sita au kulipa faini ya Sh milioni 35 kila mmoja kwa kuisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 143,442.75.

Wakati huo huo, Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani, William Haji, ambaye walishtakiwa kwa makosa hayo, ameachiwa huru.

Mattaka na wenzake wanashtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kutangaza zabuni ya ununuzi wa magari 26 yaliyochakaa na kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa amesema licha ya adhabu hiyo, washtakiwa hao pia wanatakiwa kurejesha fedha walizoisababishia serikali hasara kwa kulipa nusu ya fedha hizo kila mmoja.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na mwenzake wahukumiwa jela miaka 6 au fani ya milioni 35

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

MATTAKA WA ATCL JELA MIAKA SITA