30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Matokeo ya uchaguzi wa rais yasubiriwa

BUJUMBURA, BURUNDI

TUME ya Uchaguzi nchini Burundi inatarajiwa kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumatano iliyopita, huku Evariste Ndayishimiye, ambaye ni mgombea aliyeteuliwa na rais anayeondoka, Pierre Nkurunziza akipewa nafasi kubwa ya kutangazwa mshindi. 

Kulingana na mwaliko wa tume hiyo kwa vyombo vya habari, tangazo hilo la matokeo ya awali lilitarajiw akutolewa saa nane mchana jana kwa majira ya Burundi, na matokeo kamili yatatangazwa Juni 4. 

Matokeo ya muda yaliyochapishwa na Shirika la Habari la Taifa yalimuonyesha Ndayishimiye akiongoza kwa asilimia 80 ya kura zilizopigwa. 

Mpinzani wake mkuu, Agathon Rwasa ambaye mikutano yake ya kampeni ilihudhuriwa na umati mkubwa aliambulia takribani asilimia 20, huku wagombea wengine watano, kwa pamoja wakimudu asimilia moja. 

Msemaji wa Rwasa alisema kilichotokea ni mpango uliosukwa vyema na chama tawala wa kung’ang’ania madaraka.

Jumamosi 23, ssiku tatu baada ya upigaji kura, kiongozi wa chama kikuu cha upinzaji nchini Burundi, Rwasa, alielezea matokeo ya awali yanayompa ushindi mkubwa mgombea wa chama tawala cha CNDD-FDD,  Ndayishimiye kama “kichekesho”.

Matokeo hayo ambayo yalitangazwa Alhamisi jioni kwenye Redio na Televisheni vya Taifa yanahusu kura zilizohesabiwa katika asilimia 12 ya tarafa 119 za Burundi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Pierre-Claver Kazihise alikuwa amewatolea wito wananchi wa Burundi siku ya Alhamisi asubuhi kuwa na subira kwa kusubiri matokeo ya awali kutangazwa leo Ijumaa Mei 22 .

“Ninafutilia mbali matokeo haya. Matokeo haya ambayo wako watangaza ni matokeo bandia, hayaendani na ukweli,” Rwasa alisema Alhamisi jioni.

“Ninasema hivyo kwa sababu jana (Jumatano jioni) wakati tulianza kuhesabu kura, tulifuata taarifa kutoka vituo mbalimbali vya kupigia kura, tulikuwa tunakaribiana kwa kura na matokeo ambayo tunayo sasa ni kuwa bado tunaongoza,” aliongeza.

“Tunaweza kuonyesha kwa urahisi kuwa ni wizi wa kura. Takwimu zinazotolewa kupitia Redio na televisheni vya taifa ni matokeo ya ujanja tu,”  alisisitiza.

Matokeo hayo ya awali yalimpa mgombea wa chama tawala cha CNDD-FDD, Ndayishimiye ushindi wa asilimia 73.9 ya kura dhidi ya asilimia 24.6 alizopata Rwasa katika Wilaya ya Kabezi, mkoani Bujumbura, ambayo ngome ya kihistoria ya kiongozi wa wa chama cha upinzani cha CNL.

Chaguzi hizi, ambazo kwa ujumla zilifanyika kwa utulivu, zinaashiria mwisho wa utawala wa Nkurunziza.

AFP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles