28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mastaa wa muziki kupotezea misiba, tatizo ni nini?

SWAGGAZ RIPOTA

MIONGONI mwa  mambo yanayoonyesha upendo na ushirikiano katika jamii  yetu, ni namna watu wanavyojitokeza kwa wingi pale mmoja wao anapopatwa na matatizo na siyo kwenye matukio ya kula bata.

Gumzo kubwa wiki hii ni msiba wa baba mzazi wa nyota wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Abdu Kiba, Mzee Saleh Omar uliotokea alfajiri ya juzi katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam na akazikwa na maelfu ya wakazi wa Jiji kwenye makaburi ya Kisutu.

Baba mzazi wa Ali Kiba ambaye enzi za uhai wake alikuwa dereva wa Kimataifa, akiendesha magari makubwa yanayosafirisha mizigo nje ya Tanzania ikiwamo Afrika Kusini, aliugua kwa muda maradhi ya kiharusi yaliyosababisha kifo chake.

Shughuli za msiba huo mkubwa zilifanyika nyumbani kwake Kariakoo mtaa wa Muheza, huku viongozi wa serikali, mashabiki wengi pamoja na wasanii wachache wa Bongo Fleva wakijitokeza kuwapa nguvu na faraja wafiwa.

WASANII BONGO FLEVA MPO WAPI?

Jambo baya ambalo wasanii wa Bongo Fleva wameendelea kulifanya ni kutotokea kwenye misiba au matatizo ya wasanii wenzao. Ni tofauti kabisa na wasanii wa filamu ambao huwa wanayabeba matatizo kwa ushirikiano mkubwa.

Jaribu kukumbuka misiba inayowahusu wasanii wa filamu. Hata kama utakuwa wa muda mfupi lakini utaona jinsi wasanii wanavyojitoa na kujitokeza kwa wingi jambo ambalo mpaka sasa Bongo Muvi linawapa heshima.

Hebu vuta picha katika msiba huu wa baba wa staa mkubwa wa muziki Bongo ambaye amekuwa akijitoa katika matatizo zya wenzake, leo hii kwenye tatizo lake idadi ya wasanii wa muziki haifiki haizidi 10, hii ni aibu kwa wasanii wa Bongo Fleva yenye mamia ya mastaa.

Sura za wasanii maarufu walioonekana  katika msiba wa baba mzazi wa Kiba ni Mwana Fa, Young Killer, Mr Blue, Harmorapa, Dully Sykes, Motra The Future, Shehe Ismail ‘ Suma Lee’, Prodyuza Lamar na wengine wachache.

TATIZO NI NINI?

Hii si mara ya kwanza kwa wasanii wa muziki kutoonyesha ushirikiano kwa wenzao wanapopata matatizo. Misiba mingi inayowahusu wanamuziki, mwitikio huwa ni mdogo jambo linalozalisha swali, tatizo ni nini?

Mbona katika matukio ya kula bata, wanapeana sapoti kubwa. Hata  kwenye harakati za muziki wanaungana mkono na kupena michongo ya shoo, lakini linalokuja suala la msiba, wanajitenga, wanakuwa wazito kujitokeza msibani.

Hata kama watakosa muda wa kufika msibani, kuna  njia nyingi za kutoa pole kama vile kuwapigia simu ya kuwafariji wafiwa au hata kutoa pole kupitia mitandao ya kijamii kama ambavyo Profesa Jay, Roma na wengine amefanya mtandaoni.

TUNATOKAJE HAPA?

Kama tunahitaji ustawi wa muziki wetu basi turekebishe hili na tunaweza kutoka hapa kupitia Chama Cha Muziki wa Kizazi Kipya (TUMA), kukutana na wasanii wake na kujadiliana  kwa upana tatizo hili.

Haiwezekani kukawa na madaraja wakati wasanii wote wanafanya muziki sawa. Hatuhitaji makundi makundi na kubaguana ambako kunafanya leo hii kwenye msiba unaohusu wasanii wa kundi fulani, wasanii wanajitokeza kwa wingi lakini kuna wasanii wa kundi lingine wakipata matatizo mwitikio huwa ni mdogo.

Bila ushirikiano katika matatizo muziki wa Bongo Fleva, utachelewa kule ambako tunaelekea licha ya mafanikio mengi kuanza kuonekana sasa hivi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles