27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maspika wastaafu kukabidhiwa majoho ya Bunge

Mwandishi Wetu -Dar es Salaam

MKUTANO wa 18 wa Bunge la 11 ambao ni mahsusi kupokea na kujadili taarifa za mwaka za kamati za kudumu za Bunge, unatarajiwa kuanza leo na kumalizika Febuari 7 jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, ilieleza kuwa Bunge litakuwa na shughuli kadhaa, ikiwamo kukabidhi majoho kwa maspika wastaafu Pius Msekwa, marehemu Samuel Sitta na Anne Makinda.

 Joho alilolitumia marehemu Sitta litapokewa na mke wake Margaret Sitta kwa niaba ya familia.

Shughuli hii itafanyika katika kikao cha kwanza baada ya kipindi cha maswali. 

“Katika mkutano huu wa kumi na nane, wastani wa maswali 125 ya kawaida yanatarajiwa kuulizwa na wabunge.

“Aidha, wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku za Alhamisi Januari 30 na Febuari 6, 2020.

“Bunge pia linatarajia kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.8) wa Mwaka 2019 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.8) Bill, 2019] na Muswada wa Sheria ya Usuluhishi wa Mwaka 2020 (The Arbitration Bill, 2020).

“Katika mkutano wa kumi na nane wa Bunge, kamati za kudumu za Bunge 15 zitawasilisha taarifa za mwaka za kazi za kamati hizo kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 117(15) ya Kanuni za Bunge ambapo ni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

“Pia zipo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

“Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,” ilieleza taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles