30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MASOGANGE APEWA ONYO NA MAHAKAMA

Na KULWA MZEE – DAR ES SALAAM



MSANII Agnes Gerald ‘Masogange’, ameonywa na kutakiwa kuheshimu mahakama kutokana na kutokuwepo wakati kesi yake ya kutumia dawa za kulevya ilipotajwa jana.


Masogange alionywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, baada ya kutoonekana mahakamani hapo.

Lakini kesi hiyo ilipoitwa, Wakili wa Masogange, Nictogen Itege, alidai mshtakiwa huyo alikuwa njiani akija mahakamani hapo.
Hakimu alihoji: “Mbona wewe uko mahakamani?”
Wakili alijibu: “Tulipita njia tofauti.”


Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri alimweleza wakili huyo amwambie mteja wake aheshimu masharti ya dhamana.
Hata hivyo, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Adolf Mkini, ulidai upelelezi haujakamilika na uliomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine kwa kutajwa. Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 20, mwaka huu.


Muda mfupi baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, aliyejizolea umaarufu mkubwa nchini kutokana na kupamba video za wasanii mbalimbali, alionekana mahakamani hapo.


Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).


Pia anadaiwa kati ya Februari 7 na 14, mwaka huu, alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
Awali Masogange aliposomewa mashtaka hayo, alikana na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika ambapo hakimu Mashauri alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja alisaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10, huku akitakiwa kutokutoka nje ya Jiji la Dar es Salaam bila ya kibali cha mahakama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles