24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mashine ya Ultra sound yaibwa Hospitali ya Wilaya Bariadi

Derick Milton, Simiyu

Mashine inayotumika kupima magonjwa ya ndani na kutambua taarifa mbalimbali katika mwili wa binadamu (Ultra sound) imeibiwa katika mazingira ya kutatanisha kwenye Hospitali ya mji wa Bariadi (Somanda) mkoani Simiyu.

Mashine hiyo inadaiwa kuibiwa pamoja na kifaa chake cha kudurufu picha (printer) ambapo ilikuwa maalumu kwa matumizi ya wodi mpya ya akina mama wajawazito na iliibiwa ikiwa kwenye wodi hiyo.

Akizungumza na Mtanzania Digital Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Mike Mabimbi, amekiri kuibiwa kwa mashine hiyo ambapo amesema hadi sasa bado haijapatikana.

Mabimbi amesema kuwa baada ya kutokea kwa tukio hilo waliweza kutoa taarifa jeshi la polisi, ambapo watu 17 wakiwemo wauguzi walikamatwa kwa ajili ya mahojiano.

“Ni kweli mashine hiyo ambayo ilitolewa na wadau wa maendeleo UNFPA kwa ajili ya wodi ya akina mama tu iliibiwa katika mazingira ya kutatinisha, tayari taarifa tulitoa na polisi wanaendelea na uchunguzi,” amesema.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Mwanaidi Churu, amesema mazingira ya kuibiwa kwa kifaa hicho yameendelea kuwa magumu kutokana na watoa huduma waliokuwepo wodini siku hiyo kila mmoja kudai hajui.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles