26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mashahidi waeleza mwanafunzi alivyochapwa

Elizabeth Kilindi,Njombe

MASHAHIDI  wawili, daktari aliyemtibu pamoja na mwanafunzi mwenzake wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Njombe walivyoshuhudia aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Madeke,Hosea Manga anayedaiwa kuadhibiwa na mwalimu wake wa somo la  hisabati na kusababishiwa ulemavu wa uti wa mgongo.

Kesi hiyo namba 141 ya mwaka 2019 ya Jamuhuri dhidi ya Focus Mbilinyi, ikiongozwa na Hakimu Mkazi, Ivan Msaki huku Mwendesha Mashtaka, Elizabeti Mallya  wakati upande wa watetezi ukiwakilishwa na mawakili Octavian Mbugari na Innocent Kibadu.

Kesi hii iliendeshwa kwa takribani saa tano imeanza kwa kusikiliza ushahidi kutoka kwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Madeke, Given Nyangwinye ambaye ni shahidi namba tatu aliyekuwa anasoma shule na darasa moja na mlalamikaji  Hosea Manga aliyekumbwa na masaibu ya kuvunjika uti wa mgongo.

Akieleza mahakama, Given alidai Machi 21, mwaka huu, mwalimu Focus Mbilinyi alitoa kazi ya somo la hesabu yenye maswali 10,baadae kutoa adhabu kwa waliokosa,  huku yeye na wanafunzi wenzake akiwemo Hosea wakipokea adhabu hiyo.

Alidai yeye alikosa hesabu 6 na akatandikwa viboko vitano, huku akishuhudia mwenzake hosea aliyekosa hesabu zote akipewa adhabu ya viboko akiwa amening’inizwa kichwa chini miguu juu.

Kwa upande wa shahidi namba nne, Dk. Silvery Mwesige  kutoka Taasisi ya Mifupa (MOI) Idara ya Upasuaji wa Ubongo na Mishipa aliieleza mahakama  alianza kumuhudumia Hosea kuanzia mwanzoni mwa Aprili,2017 ambapo baada ya vipimo majibu yalionesha alikuwa na mgandamizo  sehemu ya mwisho ya uti wa mgongo  hali iliyofanya damu isiweze kufika katika eneo hilo.

Baadaye ukaibuka mvutano wa kisheria kwa mawakili watetezi ambao awali walipinga na kuhoji  uhalali wa  taarifa ya matibabu kutoka MOI,  iliyowasilishwa Dk.Mwesige kwa madai shahidi hakushiriki katika baadhi ya   vipimo vya Hosea , pingamizi lililomalizwa na  hakimu Msaki, baada ya kutoa uamuzi mdogo na ufafanuzi wa kisheria kubainisha uhalali wa taarifa na vielelezo viliyowasilishwa na Dk.Mwesige.

Dk. Mwesigwe  alipoulizwa na upande wa utetezi  aliiambia mahakama kuwa hawezi kuthibitisha adhabu ya viboko alivyopewa Hosea inaweza kuwa  ndiyo imesababisha tatizo alilonalo hivi sasa lakini amekiri kuwa adhabu ya viboko inaweza kuleta tatizo la kiafya kama la mtoto Hosea kutegemeana na nguvu na nyenzo anayotumia mtoa adhabu.

Shauri hili limeahirishwa na litaendelea kusikilizwa tena disemba 2 mwaka huu.

Mwaka 2017, kesi namba 83 ilifunguliwa na baadae kufutwa kutokana na daktari aliyemtibu Hosea Manga alitoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na  kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi licha ya kuitwa mara nane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles