26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MASHABIKI WAMTOLEA POVU DIAMOND PLATNUMZ

Na CHRISTOPHER MSEKENA

IKIWA ni siku chache zimepita toka lebo ya Universal Music Group kumtunuku msanii Diamond Platnumz tuzo ya wimbo wake wa MARRY You kufikisha mauzo ya Platnum mara sita, msanii huyo amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuwaita watoto wake (Tiffah na Nillan), mbegu.

Katika kile kilichoonekana kama ni kuwajibu wale wanaosema mtoto wake wa pili (Nillan) siyo wake, Diamond aliweka picha kwenye Instagram akiwa amewapakata watoto wake kuthibitisha kuwa wote ni wake kwa kuandika maneno yaliyopokewa kwa mitazamo tofauti.

Diamond Platnumz aliandika maneno ya Kiingereza yemye maana ya mbegu zangu, akimaanisha Tiffa na Nillan ni mbegu zake jambo ambalo lililofanya mashabiki wamjie juu kwa kutokuwa na lugha nzuri kwa wanawe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles