24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MASHABIKI UGANDA WAMTAKA DIAMOND AOMBE RADHI

KAMPALA, UGANDA


MASHABIKI wa mama watoto wa Diamond Platnumz, Zarina Hassan nchini Uganda, wamemtaka msanii huyo kutoka Tanzania kuwaomba radhi kwa kitendo chake cha kuzaa na mwanamke mwingine.

Baadhi ya mashabiki ambao walionekana wakiwa wamevaa T-shirt za Team Zari, katika tamasha la Kampala City Carnival mwishoni mwa wiki iliyopita, walibeba mabango wakimtaka Diamond kuwaomba radhi mashabiki hao.

Mwezi uliopita msanii huyo aliweka wazi kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto, kitendo ambacho Zari alionesha kuchukizwa pamoja na wale mashabiki wake wa nchini Uganda.

Hata hivyo, Diamond baada ya kuweka wazi kuwa ana mtoto na Hamisa, aliomba radhi kwa mama watoto wake, Zari, lakini mashabiki wa The Boss Lady wa nchini Uganda wanataka na wao waombwe radhi kwa kuwa wamemdhalilisha bosi wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles