MASHABIKI MAN UNITED HAWAMTAKI POGBA

0
805

MANCHESTER, ENGLAND


MASHABIKI wa timu ya Manchester United wanaofahamika kama Red Devils  jana walipiga kura ambapo asilimia 60 ya waliopiga kura walitaka viongozi wa klabu hiyo kumuuza kiungo wa timu hiyo Mfaransa, Paul Pogba.

Asilimia hiyo, ambayo ni sawa na mashabiki 2000 ya waliopiga kura hiyo, walitaka kiungo huyo kuuzwa kwa kuwa si mkubwa kuzidi klabu hiyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya Pogba (25), kuwataka mashabiki kumaliza uvumi kuhusu hoja ya kuhusishwa kuhamia Barcelona na kutofautiana na Kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho.

“Kulikuwa na majadiliano mengi,  lakini hata hivyo nipo chini ya mkataba na klabu ya Manchester United,” alisema Pogba wakati alipoulizwa katika mahojiano na Sky Germany sababu gani zilimfanya kushindwa kujiunga na klabu ya Barcelona.

“Hatima yangu ipo Manchester United, ambako sasa nacheza, lakini hakuna anayefahamu kipi kitatokea baada ya miezi michache ijayo.”

Hata hivyo, maoni ya nyota huyo yalionekana kuwachoma baadhi ya mashabiki wa timu hiyo ambao jana waliamua kupiga kura ya kumwondoa katika timu hiyo.

Baada ya juzi katika michezo ya kimataifa, Ufaransa ikifungana bao 1-1 na Ujerumani, Pogba alisema si yeye aliyetengeneza uvumi wa kuihama  Manchester United.

“Hiyo ni minong’ono tu, lakini si mimi niliyetengeneza, najaribu kupambana na hali iliyokuwapo sasa.

“Nilikuwa katika michuano ya Kombe la Dunia hivi karibuni, hivyo napambana kurejea katika kiwango changu.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here