24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Masauni azishukia shule zenye magari mabovu

Na Mwandishi Wetu- Zanzibar

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amewaonya wamiliki wa shule  ambao wanatumia magari mabovu kubebea wanafunzi.

Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu  ya usalama barabarani na udhibiti wa ajali katika Shule ya Jang’ombe.

Masauni aliwataka wamiliki wa shule  kuhakikisha wanatumia mabasi imara   kuepusha ajali.

“Wamiliki wa shule wanatakiwa wafuate sheria kwa kuacha kutumia mabasi mabovu na  kujaza wanafunzi kupita kiasi.

“Tutatumia kikosi cha usalama barabarani kuhakikisha wanafunzi wanakua salama muda wote wakiwa wanaenda shule na kurudi nyumbani.

“Nawaagiza askari wa usalama barabarani kusimamia sheria  wamiliki watakaokiuka sheria hizo waweze kuchukuliwa hatua na madereva watakaobainika kuendesha magari mabovu ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi,” alisema Masauni.

Akitoa ripoti ya matukio ya ajali za barabarani, Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Shukuru Amir Ally, alisema   ajali 229 zimeripotiwa ndani ya mwaka huu tofauti na mwaka 2017 ambako zilikuwa 391.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles