27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MASAJI HUMFANYA MTU KUWA NA HURUMA, MAONO NA UPENDO

Na FADHILI PAULO


WATU wengi wanapokabiliwa na mfadhaiko mkubwa wa kiakili na kimwili, hutafuta msaada.

Hawajui kwamba tiba mojawapo ya matatizo haya ni masaji (kuchua), ambayo ina uhakika wa uponyaji kwa karibu ya asilimia 100 bila kutumia dawa yoyote na bila madhara yoyote.

Masaji ni njia nzuri ya kuondoa msongo wa mawazo na kupigana na maradhi mengi mwilini, ukitumia viuongo vyako vya mwili bila dawa yoyote.

Masaji husaidia kuongeza kinga ya mwili, kuondoa tatizo la kukosa usingizi, kupona kiharusi (stroke), kifafa na magonjwa mengine mengi yanayohusiana na mishipa.

Masaji ni tiba inayofanywa kwa kutumia mikono tu, kinachotakiwa ni kugusagusa na kusugua juu ya mwili wako kwa namna maalumu ambayo ndiyo huamsha na kufungua mishipa na kuondoa sumu na msongo wa aina mbalimbali na hivyo kuongeza kinga ya mwili kupambana na maradhi bila kutumia dawa.

Hii ni tiba maarufu kidogo maeneo ya mijini kuliko vijijini. Pia ni huduma inayopatikana katika hoteli kubwa za kifahari maarufu SPA’s. Ingawa hawa lengo lao zaidi huwa ni lengo kubwa huwa ni kwa ajili ya kukufanya ‘u-relax’ na kupata utulivu baada ya uchovu wa shughuli za kila siku.

Hii masaji ya tiba (physiotherapy message) ni masaji maalumu kwa ajili ya wagonjwa.

 

Unayoweza kujitibu kwa njia ya kuchua mwili

 

Kuongeza kinga ya mwili

Kufanya masaji hakukufanyi ujisikie ni mtulivu pekee, bali pia kunaweza kukuongezea kinga yako ya mwili.

Masaji ya dakika 45 kwa siku imethibitika kuongeza wingi wa seli nyeupe za damu (lymphocytes) ambazo ndizo hupigana dhidi ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa mbalimbali mwilini.

Faida nyingine za kiafya ni pamoja na kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambukizi mbalimbali inayoitwa ‘cytokines.’

Pia hushusha homoni inayohusika na matendo ya mashari homoni inayoitwa ‘cortisol’.

Kipindi kimoja cha masaji kinatosha kuzalisha matokeo yanayoonekana ya kuongezeka kwa kinga ya mwili.

 

Huondoa tatizo la kukosa usingizi

Mamia ya watu wanapatwa na tatizo hili la kukosa usingizi, jambo linaloharibu ufanisi wa kazi zao kila siku.

Tatizo la kukosa usingizi linaweza kutibika kwa kufanya masaji tu kwakuwa masaji husaidia kupunguza uchovu na kuongeza uwezo wa kupata usingizi mtulivu kwa watu wa rika zote yaani watoto wadogo hadi wazee, ikihusisha wale wenye matatizo ya akili, saratani na magonjwa ya moyo, machache kati ya magonjwa mengi yanayoweza kutibika kwa masaji tu.

Tafiti nyingi zinasema masaji inao uwezo wa kuamsha mawimbi ndani ya ubongo yanayohusiana na kutengenezwa kwa usingizi mzito (delta waves) na hii ndiyo sababu kwanini wengine hupitiwa na usingizi mzito mara tu baada ya kufanyiwa masaji.

 

Huondoa mfadhaiko wa akili

Zaidi ya asilimia 32 ya watu waliojaribu tiba hii wanathibitisha kupungukiwa na kiasi kikubwa cha mfadhaiko katika miili yao, huku tafiti zaidi zikiendelea kutoa ushuhuda wa aina moja.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Harvard, umethibitisha kuwa masaji huondoa hamaki na maumivu huku ikiongeza uwezo wa kupata usingizi mzuri na wa uhakika.

Chuo kikuu cha afya cha Boston nchini Uingereza kiliona matokeo yaliyo sawa kati ya wagonjwa 60 wenye saratani ambao walifanya tiba ya masaji dakika 20 kabla ya mionzi, kuliwapunguzia kiwango cha hamaki na mfadhaiko wa akili.

Watafiti kutoka Australia wameripoti kwenye jarida la afya liitwalo ‘The Journal of Thoracic and Cardiovascular Surgery’ kuwa masaji hupunguza maumivu, hamaki na mshtuko wa mishipa baada ya upasuwaji wa moyo.

Utafiti mwingine kutoka Chuo Kikuu cha Toho nchini Japan umethibitisha kwamba masaji inayohusisha mafuta maalumu ambayo huwa na harufu ya kunukia (ya kuvutia) na ambayo ni dawa, husaidia kupunguza mfadhaiko wa kisaikolojia katika wazee wagonjwa wanaotibiwa majumbani.

 

Huondoa huzuni

Tafiti kutoka Chuo cha Afya cha Nashville’s Meharry Medical College, umethibitisha wagonjwa 43 wa Ukimwi walionyesha kuondokewa na hali zao za huzuni baada ya kufanya masaji ya mwili mzima kwa kipindi cha majuma matatu.

Profesa maarufu na mtafiti Russell Poland, Ph.D. anayehusika na magonjwa ya akili anasema: “Wakati tunaanza huu utafiti hatukutegemea kuona matokeo mazuri kiasi hiki kwa tiba hii ya masaji. Sote tulibaki na mshangao tu.”

Faida hizi zilirudiwa pia na Chuo Kikuu cha Los Angeles Calfornia nchini Marekani ambapo watu 95 waliojitolea kwa utafiti wa tiba hii ya masaji walionesha kuongezeka homoni ya ‘oxytocin’ na kupungua kwa homoni nyingine ya ‘adrenocorticotropin.’

Oxytocin inahusika na matendo ya huruma, maono, upendo na ushirikiano wa kijamii. Wakati adrenocorticotropin yenyewe huhusika na kupungua kwa mfadhaiko (stress) moja kwa moja.

 

Huondoa maumivu mwilini

Watafiti kutoka kitengo cha uuguzi cha Chuo Kikuu cha Sao Paulo nchini Brazil walitafiti wanawake 46 wajawazito waliofanyiwa masaji ya mgongo walipunguza kiasi cha maumivu wakiwa leba kwa zaidi ya asilimiaa 27.

Katika utafiti mwingine uliofanyika hospitali kuu ya Beijing nchini China, masaji nzito ilisaidia kuondoa maumivu ya mgongo kwa wagonjwa.

Kupungua kwa maumivu haya kuliripotiwa na robo tatu kati ya wagonjwa 110 waliofanyiwa utafiti huo.

Maumivu mengine yaliyoripotiwa kuondoka kwa kutumia tiba ya masaji ni pamoja na maumivu ya kichwa na maumivu ya mishipa.

 

Kuongeza uwezo wa kujiamini

Watu wengi zaidi kila kukicha wanaendelea kuitafuta huduma hii ya tiba kwa njia ya masaji wakiwa na maradhi mabalimbali katika miili yao. Madaktari wengi nao wameendelea kuwashauri wagonjwa wao kujaribu tiba hii.

Utafiti unaendelea kuwaeleimisha watoa tiba hii jinsi ya kuifanya ili kupata matokeo mazuri katika kutibu matatizo kama maumivu sugu ya misuli, matatizo yanayotokea wakati wa matibabu ya saratani, wakati wa mabadiliko yanayosababishwa na ujauzito na maradhi mengine mengi.

Matatizo mengine yanayoweza kutibika kwa kutumia masaji ni saratani ya matiti, tatizo la kufunga choo, ukichaa, maumivu ya mwili, maumivu ya kichwa, maumivu ya mifupa na kiharusi.

Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu wa tiba asili kwa maoni na ushauri wasiliana naye kupitia WhatsApp +255769142586.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles