Imechapishwa: Tue, Jan 9th, 2018

MARY J. BLIGE KUPEWA HESHIMA

NEW YORK, MAREKANI


MKONGWE wa muziki kutoka Marekani, Mary J. Blige, Alhamisi anatarajia kuwekwa nyota ya jina lake kwenye Hollywood Walk of Fame, jambo ambalo ni heshima wanayopewa wanamuziki nchini humo.

Mtayarishaji wa tukio la kihistoria amesema, Mar J Blige, ni msanii mkubwa wa kizazi hiki na kilichopita hivyo anastahili heshima hiyo na mashabiki watafurahi kuona nyota yake kwenye eneo hilo.

Sherehe hizo zitahudhuriwa na mastaa wengi wa muziki nchini humo akiwamo P Didy ambaye nyota ya jina lake iliwekwa kwenye Hollywood Walk Of Fame mwaka jana na amekuwa pamoja na Mary J Blige, toka mwanadada huyo anaanza kutoka kimuziki miaka ya 90.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

FACEBOOK

YOUTUBE

Translate »

MARY J. BLIGE KUPEWA HESHIMA