24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Marufuku wafuga nyuki wasio na vitambulisho kuingia msituni

ALLAN VICENT, SIKONGE

Mkuu wa wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora Peresi Magiri, amepiga marufuku wafuga nyuki wasio na vitambulisho kutoingia katika mapori au misitu ya hifadhi wilayani humo kwa ajili ya shughuli za ufugaji nyuki.

Ametoa agizo hilo leo Mei 23, katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) mjini hapa.

Amesema kuwa ametoa agizo hilo baada ya kukamilika kwa zoezi la ugawaji vitambulisho zaidi ya 8,000 vilivyotolewa na serikali kwa ajili ya vikundi vyote vinavyojishughulisha na ujasiriamali wilayani humo.

Magiri amebainisha kuwa wakati vitambulisho hivyo vikichangamkiwa na makundi mengi ya wafanyabiashara wadogo wadogo baadhi yao hawakuona umuhimu wake licha ya kuhamasishwa, hivyo wakapotezea wakiwemo baadhi ya wafuga nyuki.

‘Ni marufuku kwa mfuga nyuki yeyote yule kuingia katika mapori au misitu ya hifadhi kama huna kitambulisho cha ujasiriamali, na maofisa wa wakala wa Huduma za Misitu (TFS) hakuna kutoa kibali chochote kwa watu hao’, amesema.

Aidha ametoa onyo kwa viongozi wa umma watakayebainika kunyanyasa au kudai malipo yoyote kutoka kwa mjasiriamali mwenye kitambulisho hicho kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles