29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yawataja Wa-Nigeria katika uchunguzi mkubwa wa utapeli

MAMLAKA nchini Marekani imewashitaki watu 80 wengi wao wakiwa ni raia wa Nigeria  kwa tuhuma za kula njama ya kuiba mamilion ya dola, waendesha mashtaka wamesema.

Wanatuhumiwa kutumia udanganyifu wa barua pepe za kibiashara na kashfa za waathirika wa  mapenzi wengi wao wakiwa ni wazee.

Hadi sasa polisi imewakamata watuhumiwa 14 katika maeneo mbalimbali nchini Marekani, 11 kutoka Los Angeles peke yake.

Mamlaka zinasema kesi hiyo ni miongoni mwa kesi kubwa katika historia ya Marekani.

Mwanasheria wa Marekani, Nick Hanna  amesema uchunguzi huo ulioendeshwa na shirika la kijasusi la FBI ni hatua kubwa ya kuvunja mtandao wa uhalifu nchini humo.

“Kesi hii ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuwalinda Wamarekani kutoka kwenye uongo unaofanywa kwenye mitandao na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wote wanaoathiri raia wa Marekani na biashara,” aliongeza.

FBI ilianza kuchunguza kesi hiyo mwaka 2016 katika akaunti moja ya benki lakini baadae walipanua uchunguzi huo kwa ajili ya waathirika wengine wa Marekani walioko maeneo mbalimbali duniani.

Watu wote  80  wameshitakiwa kwa kula njama za kufanya udanganyifu, kula njama za kutakatisha fedha, na wizi, Ofisi ya Mwanasheria ya California ilieleza katika taarifa yake kwenye vyombo vya habari.

Raia wawili wa Nigeria, waliofahamika kwa majina ya Valentine Iro na Chukwudi Christogunus Igbokwe, ambao ni miongoni mwa waliokamatwa nchini Marekani wametajwa kuwa kwenye mtandao huo wakifanya kazi na wengine walioko Marekani na Nigeria, lengo lao likiwa ni kujipatia fedha kutoka kwa wahanga na kuzisafirisha nje.

Ofisi ya Mwanasheria ilidai watuhumiwa hao walifanikiwa kudanganya na kujipatia Dola milioni sita (£5m) kati ya Dola milioni 46 walizokuwa wamezilenga.

Mamlaka zimesema watuhumiwa wengine 66 waliobaki wanaaminika kuwa wako nje ya Marekani, wengi wao wakiwa nchini Nigeria.

Mashtaka yanadai kuwa watuhumiwa hao walitumia njia isiyo halali ya wabadilishaji fedha  kusafirisha fedha hizo kwenda Nigeria, wakikwepa kusafirisha fedha hizo moja kwa moja kupitia taasisi za kifedha kama benki.

Mamlaka imeorodhesha zaidi ya makosa 252 dhidi ya watuhumiwa hao 80.

Mmoja wa waathirika ni mwanake toka Japan anayeitwa  FK katika karatasi za mahakama, alidhurumiwa zaidi ya dola za kimarekani 200,000 baada ya kuwasiliana na tapeli aliyejitambulisha kama kapteni wa Marekani, Terry Garcia anaetaka kusafirisha almasi kupeleka Syria.

Gazeti la LA Times limeripoti kuwa mwanamke huyo alifanya malipo 35 hadi 40, huku akipokea barua pepe 10 hadi 15 kwa siku zikimtaka atume fedha kwenye akaunti Marekani, Uturuki na Uingereza kupitia washirika wa nahodha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles