27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI YATISHIA KUIWEKEA VIKWAZO IRAN

Marekani, RFI

Marekani imetishia kuweikea vikwazo Iran, baada ya Urusi kutumia kura yake ya turufu kupinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloishtumu Iran kuhusika na kuwapa silaha waasi wa Houthi katika vita nchini Yemen.

“Ikiwa Urusi itaendelea kuunga mkono vitendo vya Iran, Marekani na washirika wake watalazimika kuchukua vikwazo,” amesema Balozi wa Marekani, Nikki Haley, ingawa hakuwaambia waandishi wa habari hatua zitakazochukuliwa.

Urusi ilitumia kura yake ya turufu kupinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana Jumatatu huku Baraza hilo likielezea wasiwasi wake baada ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kupata ushahidi kwamba Iran haikuheshimu vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa kuhusu silaha kwa waasi wa Kishia wa Houthi.

Uamuzi wa rasimu uliwasilishwa na Uingereza, kwa ushirikiano na Marekani na Ufaransa ambapo kura hii ya turufu ya Urusi ni pigo kwa Marekani, ambayo imekuwa ikiomba kwa miezi kadhaa ili Iran iwekewe vikwazo na Umoja wa Mataifa. Pia Marekani inataka kurekebisha makosa ya mpango wa nyuklia wa Iran.

Januari 12, mwaka huu Rais wa Marekani, Donald Trump alikubali kwa mara ya mwisho, kuongeza muda kwa mikataba ya kiuchumi dhidi ya Iran iliyofutwa chini ya makubaliano ya 2015 kuhusu shughuli za nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu (Iran).

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles