31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI YAKIRI MATUMIZI YA SILAHA ZA KEMIKALI

DAMASCUS, Syria  

WIZARA ya Ulinzi ya Urusi imesema kwamba kwa mara ya kwanza Serikali ya Marekani imethibitisha kuwa magaidi wanaofanya mashambulizi katika Jimbo la Idlib nchini Syria, hawatumii silaha za kawaida pia wanatumia na za kemikali.

Taarifa hiyo imetolewa jana na msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Jenerali  Igor Konashenkov, wakati akizungumzia ripoti iliyotolewa na Marekani na akasema kwamba katika maelezo hayo kuna kikundi kinachoitwa Hayat Tahrir al-Sham ambacho kinashirikiana na kingine cha Jabhat al-Nusra, kikundi  ambacho kilidhibitiwa nchini Urusi kutokana na kwamba kilikuwa kikitumia silaha nzito na vifaa vilivyotengenezwa na silaha za kemikali.

“Ningependa kueleza kuwa Serikali ya Marekani kwa mara ya kwanza imekubali rasmi kuwa magaidi kutoka kundi la Jabhat al-Nusra, hawana tu silaha nzito  bali pia  ningependa kusisitiza kwamba wanatumia silaha za kemikali katika Jimbo hili  nchini Syria ili kutekeleza mashambulizi ya kigaidi, jambo ambalo  kwa mara nyingi tumekuwa tukilionya katika kulipigia kelele katika ngazi mbalimbali za kimataifa,” alisema Konashenkov.

Msemaji Mkuu huyo aliongeza kwamba tukio moja la matumizi ya silaha za kemikali lilitokea katika eneo la Khan Shaykhun lililopo katika Jimbo hilo la Idlib na lawama zikaelekezwa na Marekani kuwa lilifanywa na majeshi ya Syria  jambo ambalo halikuwa kweli.

“Wakati wapiganaji ambao kwa kweli walifanya mashambulizi hayo tulikuwa tukiwataja kuwa wana uhusiano na kundi la  Jabhat al-Nusra, lakini Marekani ilikuwa ikitilia shaka. Lakini sasa, taarifa ya Idara ya Serikali ya Marekani imeweka kila kitu wazi  kwamba  kundi la ugaidi la Jabhat al-Nusra ambalo lilikuwa na ushirikiano pia  Al-Qaeda ambalo lilisambaratishwa nchini Urusi ndilo linalotumika kutumia silaha za kemikali ili  kuteketeza maisha ya raia wasio kuwa na hatia nchini Syria,” alisema  Konashenkov.

Katika hatua nyingine, msemaji huyo aliongeza kuwa bado haijulikani kwanini Serikali ya Marekani inahitajika kutumia makombora ya gharama kubwa ya kushambulia ndege ya Syria ya Shayrat. Amesisitiza kuwa wangeweza kutumia vizuri zaidi mamilioni hayo ya dola kwa kutoa migomo kwa magaidi wa Jabhat al-Nusra.

Kwa upande mwingine Jenerali huyo ametupilia mbali madai ya Serikali ya Marekani ya kwamba majeshi ya Urusi ndiyo yalikuwa yakitumia silaha hizo katika makazi ya raia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles