33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yaimwagia sifa Zanzibar

sarah-sewallNA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya usalama wa raia, demokrasia na haki za binadamu, Sarah Sewall, amesifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kupunguza tatizo la ajira nchini. Akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha kuwawezesha wajasiriamali kilichopo eneo la Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Karume, Kisiwani Zanzibar jana, Sewall alisema SMZ inastahili pongezi katika hilo kwa kuwa imeonyesha nia ya kukabiliana na tatizo la ajira kisiwani hapa. “Kwa hiyo juhudi zinazoonyeshwa hazina budi kuungwa mkono na wapenda maendeleo na sisi Marekani tumejipanga kusaidia katika jambo hili ili kukamilisha ndoto za vijana za kujiletea maendeleo. “Nasema hivi kwa sababu Zanzibar mmepiga hatua katika kuandaa mazingira mazuri ya vijana kupata ujuzi na uelewa wa masuala ya ujasiriamali. “Nchi zilizoendelea ikiwamo Marekani, zimewekeza zaidi katika sekta binafsi zinazoendeshwa na vijana wenye taaluma za ujasiriamali, nawapongeza sana kwa juhudu mnazozifanya,” alisema Sewall. Alisema kwamba, licha ya Marekani kusimamia ukuaji wa haki za binadamu, dunia bado inasisitiza kuendelea kuwepo kwa demokrasia katika nchi za Afrika kila zinapofanya uchaguzi mkuu. Ameitaka Serikali ya Tanzania ikiwamo Zanzibar, kuhakikisha zinasimamia vizuri uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa misingi ya uhuru na haki ili uchaguzi huo umalizike kwa amani na utulivu. Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto, Ali Khamis Juma, alisema lengo la Serikali ni kuona vijana na wanawake wanajiendeleza kupitia ujasiriamali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles