30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yaidhinisha dawa Remdesivir kwa wagonjwa wa corona

WASHINGTON, MAREKANI

MAREKANI imeidhinisha majaribio ya dawa ya dharura itakayotumika kwa wenye virusi vya corona.

Hatua hiyo imekuja wakati  pia majimbo zaidi nchini humo yakilegeza masharti ya kutotoka nje licha ya vifo vitokanavyo na virusi hivyo kuzidi kuongezeka.

Kuidhinishwa kwa dawa hiyo ni hatua ya hivi karibuni ya juhudi za dunia kupata tiba kamili na chanjo ya virusi vya corona vilivyowaacha nusu ya watu duniani wakibakia nyumbani, kutikisa uchumi wa dunia na kuwaambukiza watu zaidi ya milioni 3.3 ulimwenguni.

Dawa hiyo inayojulikana kama Remdesivir, iliyotengenezwa kupambana na ugonjwa wa ebola iliidhinishwa baada ya majaribio kadhaa kuonesha imewasaidia wagonjwa mahututi wa COVID 19 kupata nafuu. 

Marekani ina wagonjwa milioni 1.1 wa virusi vya corona na kurekodi vifo 65,000 hali inayomfanya rais Donald Trump kuwa mbioni kubadili hali wakati taifa hilo lilio na uchumi mkubwa duniani likirekodi idadi kubwa ya watu waliokosa ajira kutokana na janga la virusi hivyo.

Wakati huo huo Hakimu wa mahakama kuu nchini Ufilipino amesema takriban wafungwa 10,000 wameachiwa huru wakati taifa hilo likijitahidi kudhibiti virusi vya corona katika magereza yake yaliojaa wafungwa. 

Hatua hii inafuatia maagizo yaliotolewa ya kuwaachia huru wafungwa wanaosubiri kushitakiwa kwasababu hawakuweza kulipa dhamana, alisema hakimu huyo Mario Victor Leonen alipozungumza na waandishi habari. Msongamano katika magereza nchini Ufilipino ni tatizo kubwa tangu rais Rodrigo Durtete alipoanzisha hatua za kuwafuatilia wafanyabiashara ya madawa ya kulevya mwaka 2016. 

Ugonjwa wa COVID 19 umeripotiwa katika baadhi ya magereza yaliojaa watu na kuwaathiri wafungwa pamoja na maofisa wa magereza nchini Ufilipino. 

Kulingana na mfumo wa magereza nchini humo kukaa umbali wa mita moja na nusu kati ya mtu na mtu ni jambo lisilowezekana kutokana na wafungwa kurundikana mara tano ya kiwango kinachohitajika katika chumba kimoja cha magereza nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles