33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani kutumia dawa ya ebola kutibu corona

BBC, Marekani

Wakati dunia ikihangaika walau kupata hata chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, nchini Marekani inadaiwa kuvumbuliwa dawa inayopunguza muda wa dalili za virusi hivyo kuonekana kutoka siku 15 hadi siku 11.

Kwa mujibu wa maofisa wa Marekani, dawa hiyo inayoitwa Remdesivir, upo ushahidi wa wazi kwamba dawa hiyo inaweza kuwasaidia wagonjwa wa corona kupona virusi hivyo.

Dawa ya remdesivir inapunguza muda wa dalili kutoka siku 15 hadi siku 11 kulingana na majaribio yaliofanywa katika hospitali katika maeneo mbalimbali duniani.

“Maelezo kamili hayajachapishwa, lakini wataalamu wanasema kwamba yatakuwa matokeo bora iwapo yatathibitishwa ingawa si suluhu ya moja kwa moja ya ugonjwa huo.

“Dawa hiyo ina uwezo wa kuokoa maisha, kuondoa shinikizo katika hospitali na kusaidia baadhi ya masharti ya kutotoka nje kuondolewa,” imesema taarifa hiyo.

Inaelezwa Remdesivir kwa mara ya kwanza ilitengenezwa kutibu ugonjwa wa ebola. Kwa hiyo ni dawa ya kukabiliana na virusi na inafanya kazi kwa kushambulia ‘enzymes’ ambazo virusi vinahitaji ili kuweza kuzaana ndani ya seli ya mwili wa mwanadamu.

Majaribio hayo yalisimamiwa na taasisi ya Marekani kuhusu uzio na magonjwa ya maambukizi (NIAID) na watu wapatao 1.063 walishiriki. Baadhi ya wagonjwa walipatiwa dawa hiyo huku wengine wakipata tiba inayofanana na hiyo.

Dk. Anthony Fauci ambaye anaongoza Shirika la NIAID anasema takwimu zinaonyesha kwamba Remdesivir ina nguvu za wazi kwamba inaweza kupunguza dalili na kusaidia mtu kupona kwa haraka.

“Matokeo hayo yanathibitisha kwamba dawa hiyo inaweza kuzuia virusi hivyo na sasa tuna uwezo wa kutibu wagonjwa,” amesema.

Hata hivyo, pia inaonyesha kwamba remdesvir si suluhu wakati huu na faida ya kumsaidia mtu kupona ni asilimia 30. Dawa nyingine zinazochunguzwa kutibu corona ni pamoja na zile za malaria na HIV ambazo zinaweza kushambulia virusi hivyo pamoja na kuwa dawa zinazoweza kulinda kinga ya binadamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles