24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI KUAMUA JUU YA USHURU WA BIDHAA ZA CHUMA KUTOKA EU

BRUSSELS, UBELGIJI



VIONGOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) wameupokea kwa shingo upande hatua ya Marekani kusitishia kwa muda kuamua juu ya ushuru wa bidhaa za chuma cha pua na bati kwa nchi hizo pamoja na Mexico na Canada.

Rais Donald Trump aliahirisha kuchukua hatua ya kuweka au kufuta ushuru huo hadi Juni Mosi huku akisema yamefikiwa makubaliano ya kuziondolea moja kwa moja ushuru kama huo Argentina, Australia na Brazil.

Uamuzi huo umepitishwa saa machache kabla ya kumalizika muda uliopangwa wa kusimamishwa kwa muda ushuru huo kwa nchi hizo.

Akitangaza uamuzi huo Rais Donald Trump alisema:”Leo (juzi) `natetea usalama wa taifa la Marekani kwa kuzitoza ushuru bidhaa za chuma cha pua na bati zinazoagizwa kutoka nje.

“Tutatoza ushuru wa asilimia 25 kwa chuma pua na asilimia 10 kwa bati, ikiwa bidhaa hizo zitavuka mpaka wetu. Tunahitaji chuma pua bila ya shaka lakini tunataka tupatiwe bidhaa hizo kwa njia za haki na tunataka wafanyakazi wetu walindwe na tunataka kampuni zetu pia zilindwe.”

Hata hivyo, EU unasema hatua ya Rais Trump kuahirisha uamuzi kuhusu ushuru wa bidhaa hizo inarefusha mashaka.

“Uamuzi wa Rais wa Marekani unazidisha hali ya wasi wasi katika masoko ya dunia, ambayo tayari umeathiri maamuzi ya kibiashara” walisema viongozi wa Halmashauri Kuu ya EU katika taarifa yao.

“Umoja wa Ulaya unastahili kuondoshewa moja kwa moja ushuru huo kwa sababu EU hauwezi kuwa tisho kwa usalama wa Marekani.”

Taarifa ya Halmashauri Kuu ya EU imeongeza kusema majadiliano pamoja na Marekani yataendelezwa, lakini hawako tayari kuzungumza katika hali ya vitisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles