30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mapambano ya wauza unga yasababisha jeshi kumwachia mtoto wa El Chapo

CULIAC’AN, MEXICO

VURUGU kubwa zimeibuka kaskazini mwa Mexico baada ya askari kumkamata mtoto wa mfanyabiashara nguli wa dawa za kulevya, Joaquín “El

Chapo” Guzmán ambaye anatumikia kifungo.

Mapigano hayo yaliyochukua saa kadhaa  na kusababisha jeshi kuingilia kati baada ya Ovidio Guzmán López kukamatwa kwenye doria ya kawaida katika mji wa Culiacán, yalisitishwa baada ya kijana huyo kuachiwa huru.

Mamlaka za nchini humo zimeeleza kuwa Ovidio Guzman aliachiwa huru muda mfupi baadae ili kuzuia vurugu kuendelea.

Vurugu hizo zilisababisha mitaa kufungwa huko Culiacán.

Picha za video zilionyesha wanaume wenye silaha nzito wakiwa wanapambana na polisi.

Hali kadhalika picha hizo zilionyesha  miili ya watu pamoja na magari yaliyochomwa moto yakiwa yamefunga barabara.

Waziri wa ulinzi nchini Mexico, Alfonso Durazo alisema oparesheni hiyo ilianza kwa  kutumia silaha wakati wakiwa ndani ya nyumba ambayo Guzmán alikuwa ameshikiliwa.

Kwamba walilazimika kutumia silaha kwa ajili ya usalama wao.

“Walifanikiwa kumkamata Ovidio Guzman lakini baadae aliachiwa huru, ili kuzuia mapigano hayo kuendelea katika eneo hilo na kuzuia mauaji ya watu ilibidi wamuachie huru ili kurejesha amani katika mji huo”, alisema Durazo.

Ovidio aliwahi kukamatwa Marekani mwaka 2017.

Rais wa Mexico, Andrés Manuel López Obrador alisema kuwa ataandaa mkutano na kamati ya usalama kujadili suala hilo.

Obrador alichaguliwa katika jukwaa la kukabiiana na dawa za kulevya nchini humo na kuanzisha jeshi la usalama la kitaifa ili kupambana na wasambazaji hao.

Mamlaka zinaeleza kuwa chini ya uongozi wa El Chapo, wafanyabiashara wa dawa za kulevya wa Sinaloa ndiye alikuwa msambazaji mkubwa wa dawa za kulevya kuelekea Marekani

Kwa sasa El Chapo akiwa gerezani, wafanyabiashara hao walidaiwa kusimamiwa na Ovidio Guzmán, ambaye anashutumiwa kwa usambazaji wa dawa za kulevya nchini Marekani.

Inaelezwa kuwa ni kundi la wafanyabiashara wa dawa za kulevya ndio walioanzisha mashambulizi makubwa kwa polisi ili kujaribu kumuokoa kiongozi wao, Ovidio Guzman.

Inalezwa kuwa baadhi  walivamia ofisi za Mwendesha Mashtaka na kuendesha mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya mji.

Ovidio Guzmán, alisema kuwa akiwa na miaka 20 aliaminika kuwa kiongozi wa kundi la Sinaloa , baada ya baba yake kufungwa.

Vyombo vya habari vya Mexico vimeripoti kuwa Ovidio Guzmán anatafutwa Mareani kwa mashtaka yanayohusika na dawa za kulevya.

Hakukuwa na taarifa rasmi ya idadi ya watu ambao wamekufa katika mapigano hayo.

Maafisa wa serikali waliliambia shirika la habari la Reuters kuwa baadhi ya maafisa walikuwa wamejeruhiwa bila kutaja idadi yao au kueleza hali yao ilikuaje.

Mkuu wa ulinzi wa jimbo la Sinalo, Cristobal Castaneda alikiambia kituo cha televisheni cha Televisa Network kuwa watu wawili wameuawa na wengine 21 kujeruhiwa.

El Chapo mwenye umri wa miaka 62 alikutwa na hatia mjini New York kwa makosa 10, yakiwemo usafirishaji wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha. Kwa sasa amefungwa gerezani chini ya ulinzi mkali, awali aliwahi kutoroka mara mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles