26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAOMBI 25 YAFUNGULIWA MAHAKAMA YA MAFISADI

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema tangu Mahakama Kuu Divesheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi), ianzishwe, imesajili maombi 25.

Kauli hiyo aliitoa juzi mjini hapa alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake ya mwaka wa fedha 2017/18 , ambapo alisema kati ya maombi yaliyosajiliwa na divisheni hiyo, 20 yamesajiliwa Dar es Salaam, matatu Mtwara, Moja Iringa na jingine moja Tabora.

“Katika maombi 25 yaliyosajiliwa, 13 yametolewa uamuzi na mengine yanaendelea kufanyiwa kazi,” alisema Profesa Kabudi.

Alisema kila Kanda ya Mahakama Kuu ni masjala ndogo ya divisheni hiyo.

Alizungumzia pia urejeshwaji wa wahalifu na ushirikiano na mataifa kwenye makosa ya jinai, alisema Tanzania ilipeleka nje ya nchi maombi mawili ya kukusanya ushahidi na vielelezo ambayo yanaendelea kushughulikiwa.

Alisema pia Tanzania ilipokea maombi manne ya kurudisha watuhumiwa kwenye nchi walizofanya uhalifu.

Alisema maombi matatu yanaendelea kufanyiwa kazi na mengine mawili yalikataliwa kwa kutokidhi matakwa ya kisheria.

Alisema pia Tanzania ilipokea maombi 12 ya kukusanya ushahidi na vielelezo na kwamba manne kati yake yalishughulikiwa na nane yanaendelea kufanyiwa kazi.

Pia alisema mapitio yamefanywa katika Bodi za Wadhamini za taasisi zilizosajiliwa ili kuzifahamu uahai wake na jumla ya 181 zilifutwa.

Alisema katika kipindi cha Julai 2016 hadi Machi 2017 kulikuwa na mashauri 463 ya ujangili kati ya mashauri hayo 158 yalihitimishwa kwa washtakiwa kutiwa hatiani na kupewa adhabu za vifungo na kulipa faini ya Sh 811 milioni.

Kwa mwaka wa fedha 2016/17, wizara hiyo iliidhinishiwa na Bunge Sh bilioni 155.192, kati yake mishahara ikiwa ni Sh bilioni 67.328, matumizi mengineyo Sh bilioni 50.404 na fedha za miradi ya maendeleo Sh bilioni 37.919.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa, akitoa maoni ya kamati yake alisema Serikali ikamilishe kwa haraka utekelezaji wa mpango wa kuhamia Dodoma mapema iwezekanavyo ili kutekeleza uamuzi wa Serikali kuhamishia makao makuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles