30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Maofisa 59 polisi wapandishwa vyeo

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, akimvisha nishani IGP mstaafu, Omari Mahita, ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa kuwa IGP wa kwanza Tanzania kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo, Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, akimvisha nishani IGP mstaafu, Omari Mahita, ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa kuwa IGP wa kwanza Tanzania kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo, Dar es Salaam jana.

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

RAIS John Magufuli amewapandisha vyeo maofi sa 59 wa Jeshi la Polisi nchini, huku pia akiwateua viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, iliwataja maofi sa wa polisi waliopandishwa vyeo kuwa ni pamoja na 25 ambao wametoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).

Katika kundi hilo, wamo Essaka Mugasa, Adamson Mponi, Charles Kenyela, Richard Revocatus, Geofrey Kamwela, Lucas Mkondya, John Gudaba, Matanga Mbushi, Frasser Kashai, Ferdinand Mtui na Germanus Muhume.

Wengine ni Fulgence Ngonyani, Modestus Lyimo, Mboje Kanga, Gabriel Njau, Ahmed Msangi, Anthony Rutashubulugukwa, Dhahir Kidavashari, Ndalo Shihango, Shaaban Hiki, Simon Chillery, Leonard Paul, Ahmada Khamis, Aziz Mohamed na Juma Ally.

Rais Magufuli pia amewapandisha vyeo maofi sa wengine wa jeshi hilo 34 kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).

Waliopandishwa vyeo hivyo ni pamoja na Fortunatus Musilimu, Goyayi Goyayi, Gabriel Mukungu, Ally Ally, Edward
Bukombe, Sifael Mkonyi, Naftari Mantamba, Onesmo Lyanga, Paul Kasabago, Dadid Hiza na Robert Mayala.

Wengine ni Lazaro Mambosasa, Camilius Wambura, Mihayo Msikhela, Ramadhani Mungi, Henry Sikoki, Renata
Mzinga, Suzan Kaganda, Neema Mwanga, Mponjoli Lotson, Benedict Wakulyamba, Wilbroad Mtafungwa, Gemini Mushi na Peter Kakamba.

Pamoja na hao ambao uteuzi wao umeanza tangu juzi, pia wapo Ramadhan Hassan, Christopher Fuime, Charles Ulaya, Gilles Muroto, Mwamini Lwantale, Allute Makita, Kheriyangu Khamis,
Nassor Mohammed, Salehe Salehe na Mohamed Mohamed.

Kwa upande wa watendaji, Rais Magufuli amemteua Prof. William Mahalu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na uteuzi wake umeanza jana.

Rais Magufuli pia amemteua Prof. Mohamed Janabi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Awali Profesa Janabi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo.

Katika uteuzi huo, Dk. Charles Majinge anakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, huku Dk. Julius Mwaiselage anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Prof. Angelo Mapunda ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu, huku Sengiro Mulebya akiteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu.

Wengine walioteuliwa ni pamoja na Oliva Mhaiki ambaye anakuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) pamoja na Mwalimu Winifrida Rutaindurwa ambaye anakuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles