24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Maofisa 16 wa FIFA kufikishwa kizimbani

CallejasZURICH, USWISI

MAOFISA 16 wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), wanatarajia kufikishwa kizimbani kutokana na kuhusika na tuhuma za rushwa baada ya uchunguzi wa kina ambao unafanywa na waendesha mashtaka wa nchini Marekani.

Wanaotarajiwa kufikishwa kizimbani ni pamoja na maofisa wa ngazi ya juu wa Kamati ya uongozi ambao wapo madarakani kwa sasa na wale waliostaafu, akiwemo Rais wa Chama cha Soka cha Honduras, Rafael Callejas.

Mwanasheria Mkuu nchini Marekani, Loretta Lynch, amesema katika kipindi cha uongozi wao maofisa hao walikula njama ya kula rushwa ndani ya shirikisho hilo ya dola za Kimarekani milioni 200.

“Baraza la wazee wa mahakama wa Brooklyn wamerudisha mashtaka 92 katika mashtaka makuu dhidi ya washtakiwa wapya 16, wote ni maofisa wa sasa na wale wa zamani wa shirikisho hilo.

“Kila mmoja katika hao maofisa wameshtakiwa kwa kula njama ya kujipatia fedha kwa udanganyifu na makosa mengine kwa kutumia nafasi zao kujinufaisha wenyewe.

“Ngoja niweke wazi kwamba uvunjifu wa uaminifu hapa ni ufisadi wa hali ya juu na kiwango cha rushwa wanachotuhumiwa hapa kimepitiliza.

“Ujumbe ni kwamba kila mtuhumiwa aliyebaki ambao tumewahifadhi wakidhani wanaweza kukwepa, uchunguzi bado unaendelea na wataendelea kupatikana,” alisema Lynch.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles