25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Manula, Juma Abdul warejeshwa timu ya Taifa

Theresia Gasper -Dar es salaam

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Etienne Ndayiragije, ametaja kikosi cha wachezaji 32, kitakachoshiriki michuano ya Cecafa inayotarajia kufanyika nchini Uganda, huku akiwarejesha wachezaji Aishi Manula pamoja na Juma Abdul.

Michuano hiyo inatarajia kuanza kufanyika Desemba 9 hadi 19 mwaka huu nchini humo, ambako zitashirikisha timu 10.

Timu hizo zipo kwenye makundi matatu ambako Kundi A ni Uganda, Burundi, Ethiopia, na Eritrea, huku Kundi B zikiwa DRC Congo, Sudan, Sudani Kusini na Somalia na Kundi C ni Kenya, Tanzania, Djibout na Zanzibar.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ndayiragije alisema anaamini kikosi hicho kitafanya vizuri katika michuano hiyo kwa kuleta ushindani wa hali ya juu.

“Tunatarajia kuanza mazoezi Jumapili kabla ya kwenda Uganda ambako michuano hiyo itafanyika kwani tunahitaji tukafanye vizuri ili tuitangaze vizuri Tanzania,” alisema.

Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika nchini Kenya mwaka 2017, ambako Kilimanjaro Stars ilitolewa hatua ya awali baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Rwanda, ambao walimaliza wakiwa na pointi nne, baada ya kucheza michezo minne na kutoa sare moja huku ikipoteza miwili na kushinda mmoja katika Kundi A.

Wachezaji walioitwa ni pamoja na makipa Juma Kaseja(KMC), Metacha Mnata (Yanga), Aishi Manula (Simba)na David Kisu (Gor Mahia).

Mabeki ni Juma Abdul, Kelvin Yondan (Yanga), Nickson Kibabage(Difaa El Jadida, Morocco), Gadiel Michael, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, (Simba) Mwaita Gereza (Kagera Sugar), Bakari Mwamnyeto (Coastal Union).

Viungo ni Abdulmajid Mangalo (Biashara United), Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga (Simba), Fred Tengelu, Paul Nonga (Lipuli FC), Zawadi Mauya (Kagera Sugar) Idd Seleman, Salum Abubakar, ‘Sure Boy’, (Azam FC), Kelvin John (Football House), Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania), Mkandala Cleofance (Tanzania Prisons) Jafar Kibaya (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni Eliud Ambokile (TP Mazembe DR Congo), Miraji Athuman (Simba), Yusuph Mhilu (Kagera Sugar), Eliuter Mpepo (Buildcon, Zambia) Shaban Chilunda (Azam FC), Kikoti Lucas (Namungo FC).

Manula na Andul ni wachezaji ambao walikuwa hawapo kwenye kikosi cha timu hiyo na kosa michezo kadhaa jambo ambalo liliwafanya mashabiki walizungumzie mara kwa mara, lakini sasa mwalimu ameamua kukata kelele za mashabiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles