Imechapishwa: Thu, Sep 14th, 2017

MANJI URAIANI!

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwachia huru Mfanyabiashara Yusuph Manji, aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kusema hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Manji ameletwa mahakamani hapo leo Septemba 14, kwa hati ya dharura akitokea gerezani Keko kutokana na uamuzi huo wa DPP.

Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi aliiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo chini ya Kifungu Namba 91 (i), cha mwenendo wa makosa ya jinai kinachompa mamlaka DPP kufuta kesi endapo ameona hana haja ya kuendelea nayo.

Katika kesi hiyo, Manji na wenzake Deogratius Kisinda (28), Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43), walikuwa wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya uhujumu uchumi na Usalama wa Taifa kwa kukutwa na mihuri na vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

MANJI URAIANI!