Imechapishwa: Mon, Jul 30th, 2018

MAN UNITED KUMKOSA MATIC

MICHIGAN, MAREKANI

UONGOZI wa klabu ya Man United, umethibitisha kuwa, utamkosa kiungo wake Nemanja Matic mwanzoni mwa msimu huu kutokana na kufanyiwa upasuaji.

Kiungo huyo alipata majeraha katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi huku akiwa na timu ya taifa ya Serbia, lakini timu hiyo ilikuja kufungashiwa virago katika hatua ya makundi.

Kocha wa Man United, Jose Mourinho, amedai mchezaji huyo atakuwa nje mwanzoni mwa msimu huu wa Ligi hata hivyo hajui atakuwa nje kwa kipindi gani.

“Matic amewasili kutoka kwenye michuano ya Kombe la Dunia lakini hayupo sawa kutokana na kupata majeraha, hivyo hawezi kuwa na sisi mwanzoni mwa msimu kutokana na tatizo hilo, lakini sijui atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi gani,” alisema Mourinho.

United inazidi kuwa katika wakati mgumu kwa kumkosa mchezaji huyo, huku jana alfajiri ikikubali kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Liverpool. Kocha huyo akadai kuwa kichapo hicho kimechangia na kutofanya usajili wa nguvu.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

MAN UNITED KUMKOSA MATIC