24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mamlaka Dawa za Kulevya yatahadharisha vitafunwa vya mtaani

Na CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

JAMII imetakiwa kuwa makini na vitafunwa vinavyouzwa mitaani, ikiwamo keki na kashata kwakuwa kumeibuka mtindo mpya wa kuchanganya bangi na dawa nyingine za kulevya.

Akizungumza na MTANZANIA jana katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasaba, ofisa kutoka Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya (Adu), Sajenti Chad Ngatunga, alisema kadiri siku zinavyokwenda, watumiaji wa mihadarati wamekuwa wakitumia mbinu mpya ili kutenda uhalifu.

Alisema watumiaji wa mihadarati hiyo wanafahamu maeneo wanayouziwa bidhaa hizo zilizochanganywa na dawa.

“Wapo wengine wanakwenda duka la madawa wananunua dawa kisha wanahangaika na kimiminika aina ya Energy na kujikuta wakilewa kupitiliza,” alisema Ngatunga.

Alisema mabadiliko ya sheria yaliyofanyika mwaka 2015 kuhusu bangi na dawa za kulevya yameongeza adhabu za matukio hayo ili kukomesha vitendo hivyo ndani ya jamii.

 “Mabadiliko ya sheria kwa sasa yamebadilika, hivyo kwa anayekamatwa na dawa za kulevya gramu 20 anaweza kufungwa maisha au adhabu kali na akikutwa na bangi kilo 50 anazuiwa dhamana,” alisema Ngatunga.

Alisema mwaka huu kuna binti alikwenda kumtembelea rafiki yake wa kiume, hakumkuta, akaangalia ndani ya friji na kukuta keki akala, lakini ilikuwa na dawa za kulevya.

“Baada ya kula ile keki akaanza kulegea na kukimbizwa hospitali,  polisi walipopewa taarifa wakafika eneo la tukio na wakaichukua keki hiyo, ilipopimwa walibaini ilichanganywa na dawa za kulevya,” alisema Ngatunga.

Alisema utafiti mdogo walioufanya wamebaini watu wengi hawana uelewa kuhusu dawa za kulevya na athari zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles