30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Malema mahakamani kwa uchochezi

julius-malemaJOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

MWANASIASA wa upinzani nchini Afrika Kusini, Julius Malema, amefikishwa mahakamani jana kwa mashtaka ya kuchochea watu watwae kwa nguvu mashamba yanayomilikiwa na wazungu.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni mwakani kumpa Malema muda wa kupinga kipengele cha katiba kilichotumiwa enzi za ubaguzi wa rangi kumshtaki.

Malema alifika katika mahakama ya mji wa Bloemfontein kutokana na hotuba aliyotoa mwaka 2014.

Katika hotuba hiyo alisema: “Tutainyakua ardhi ambayo haijakaliwa kwa sababu tunaitaka ardhi hiyo. Ili sisi tule, ni lazima tuinyakue ardhi hiyo. Ili sisi tufanye kazi, ni lazima tuinyakue. Ninatoka Seshego. Kama kuna ardhi haina watu eneo langu, nitaenda niinyakue. Ni lazima uende ufanye hivyo hivyo katika eneo unalotoka.”

Malema alifika katika mahakama nyingine kwa mashtaka kama hayo wiki iliyopita, kufuatia hotuba aliyotoa Juni kuwa wazungu hawastahili kudai kumiliki ardhi, kwa sababu waliikuta ikimilikiwa na weusi ambao ndio wengi nchini hapa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles