26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Makundi 92,491 yawezeshwa kupata haki kupitia msaa wa sheria

Ferdnanda Mbamila, Dar es Salaam

Kituo cha msaada wa sheria  kwa wanawake, watoto na wakimbizi (WLAC), katika kipindi cha miaka 30 kimewezesha makundi hayo 92,491 kupata haki kupitia msaada wa sheria.

Kesi zilizoripotiwa zaidi Kwa kipindi hicho ni ndoa, ardhi, mirathi na matunzo ya watoto.

Wakili wa Kituo hicho, Theodorothia Muhulo amesema awali kulikuwa na mabadiliko makubwa ya uelewa wa wanawake  kuhusu haki zao kati ya mwaka 2009 na 2018.

Amesema kwa wakati huo idadi ya wanawake wanaodai haki zao katika kesi za ndoa  walikua wakiondoka katika ndoa.

“Idadi iliongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo wanawake walikua wakiondoka katika ndoa bila kudai mchango wao wa mali zilizopatikana wakati wa ndoa,” amesema Theodorosi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles