MAKONTENA YA MAKONDA YAKOSA WATEJA KWA MARA NYINGINE

0
695

 

Makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda yameshindwa kununuliwa kwa mara nyingine kutokana na waliojitokeza katika mnada huo kutofikia bei iliyokusudiwa.

Makontena hayo ambayo yanapigwa mnada na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart kwa idhini ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) yamenadiwa  leo  kwa mara nyingine katika  ghala la Dar es Salaam Inland Container Deport (DICD) bandari eneo la Kurasini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevera amewaambia waandishi wa habari kwamba licha ya makontena ya Makonda pia wanafanyamnada kwa vitu vingine mbalimbali zikiwemo samani za ndani.

“Hatukuuza ‘fanicha’ peke yake tumekuja kuuza vitu mbalimbali yakiwemo magari yaliyopata wateja lakini kwa makontena yenye vitu mbalimbali yameshindikana kufikia bei elekezi.

“Tunasubiri wenzetu wa TRA watupe muongozo zaidi kwa maana kuna watu wanafika hadi milioni 20 na 40 lakini bado bei hazifikii bei elekezi maana tunapouza mali za serikali lazima tunakuwa na ‘reserve price”, alisema Kevera.

Mnada wa kwanza wa makontena hayo ulifanyika Agosti 25 ambapo siku moja baadaye mkuu wa mkoa ambaye makontena yake yanapigwa mnada alipokuwa wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera alifanya ibada  maalum  ya kumuomba Mungu ili wanaofanya mnada huo wasipate wateja.

Makonda alishiriki ibada hiyo  katika Kanisa la Anglikana ambapo ibada hiyo iliyoongozwa na Mchungaji, Sabimbona Rushashi, Mjini Ngara. “Amelaaniwa mtu yule atakaye nunua ‘furniture’ samani za walimu. Nimefanya ibada maalumu leo (jana) ya kuhakikisha makontena hayo hayapati wateja kwa sababu naamini Mungu alinipa kwa ajili ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wanaofanya kazi katika mazingira magumu ikiwa ni jitihada zangu binafsi.

Mnada wa pili ulifanyika septemba mosi mwaka huu, hata hivyo wanunuzi waliofika katika mnada huo hawakufika bei elekezi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here