MAKONTENA YA MAKONDA YADODA TENA

0
333
MNADA: Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Scholastica Kevela (katikati), akiongoza mnada wa makontena yenye samani mbalimbali zinazodaiwa kuingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Dar es Salaam jana. PICHA:IMANI NATHANIEL.
MNADA: Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Scholastica Kevela (katikati), akiongoza mnada wa makontena yenye samani mbalimbali zinazodaiwa kuingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Dar es Salaam jana. PICHA: IMANI NATHANIEL.

Na Grace Shitundu


WAKATI makontena 20 yenye samani za shule ambayo yanadaiwa kuwa ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yakipigwa mnada kwa mara ya tatu jana, wanunuzi wameshindwa kufika bei.

Makontena hayo ambayo yanapigwa mnada na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart kwa idhini ya Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) yalinadiwa jana  katika  ghala la Dar es Salaam Inland Container Deport(DICD)  eneo la  bandari Kurasini.

Kontena moja tu lenye namba 3200018 ndilo lililonekana kugombewa baada ya wanunuzi kuweka dau la kuanzia milioni 15 hadi 40 tofauti na makontena mengine ambayo dau lilikuwa ni kuanzia milioni tano na 18.

Mnada huo ambao ulianza  takribani saa  4:16  pamoja   na  kuwepo kwa makontena hayo ambayo yanadaiwa kuwa ya Makonda  pia kulikuwa na  makontena mengine ambayo yalikuwa na vifaa vingine vilivyokuwa vikiuzwa kama matrekta, magari  na vifaa vya kilimo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevera alisema katika mnada huo wamefanya mnada wa vitu mbalimbali.

“Hatukuuza fanicha peke yake tumekuja kuuza vitu …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here