MAKONTENA YA MAKONDA, SHERIA IFUATE MKONDO WAKE

0
809

MWANDISHI WETU


SHERIA ni msumeno, kwani unakata pande zote pasina kuonea upande mwingine hivyo ndivyo inapaswa kuwa katika mgogoro uliopo dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mamlaka ya Mapato Tanznaia (TRA) na Waziri wa Fedha ana Mipango, Dk Philip Mpango.

Mgogoro ambao unatokana na makontena ambayo yaliingizwa nchini kwa jina Paul Makonda ambaye alidai kuwa yana samani za kupeleka mashuleni ambazo ni msaada kutoka kwa wadau nje ya nchi.

Baada ya kufika katika Bandari ya Dar es Salaam, TRA waligoma kuachia makontena mpaka yalipiwe kodi kama sheria inavyowataka hasa ukilinganisha yaliingizwa nchini kwajina la Makonda na sio kwa jina la ofisi yake ambapo kwa mijibu wa sheria yangeweza kuondolewa kodi.

Kutokana na hali hiyo TRA ilimtaka Makonda kulipa kodi ili kuweza kuchukua makontena yake ambayo ni takribani 20 lakini ameshindwa kufanta hivyo hivyo mamlaka hiyo kuchapisha tangazo kwenye gazeti la Serikali la Daily News Mei 12 lililowataka wamiliki wa mali zilizokaa bandarini kwa zaidi ya siku 90 kujitokeza kuzilipia.

Hivi karibuni wakati Makonda alikaririwa na chombo cha habari akitoa onyo kwa mtu atakayenunua makontena yake 20 atalaaniwa yeye na uzao wake.

“Nimekwenda katika ibada ya Jumapili katika Kanisa la Anglikana mjini Ngara, nimefanya ibada maalumu kuhakikisha makontena hayo hayapati wateja kwa kuwa naamini Mungu alinipa kwa ajili ya walimu wa mkoa wangu,” alisema Makonda.

Juzi Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo yalipohifadhiwa makontena hayo katika Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD) aliagiza kupigwa mnada kwa makontena 20 yaliyoingizwa na Makonda.

Aliiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia Sh bilioni 1.2.

“Na Sheria za nchi hazichagui sura wala cheo cha mtu, na mimi ndiyo nilichoapa. Niliapa kutekeleza sheria za nchi kwanza, nililotaka kusema kamishna katika suala la kusimamia sheria za kodi ya forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, sheria zetu za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kadhalika, simamia sheria bila kuyumba,” alisema Dk. Mpango.

Sheria haichagui mtu wa kumsulubu awe mwananchi wa kawaida au kiongozi hivyo kama inasema mtu ukipitisha mzigo baranbdari lazima ulipie kodi haina budi kufuatwa… hakuan haja ya kuendelea kulumbana wakati kila kitu kinajieleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here