31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Makondakta, madereva kubadilishiwa sare

Na Asha Bani -Dar es salaam

MADEREVA wa daladala  na makondakta wao  Mkoa wa Dar es Salaam, wako mbioni kubadilishiwa mwonekano mpya wa sare zao wanapokuwa kazini.

Hatua hiyo, imeelezwa kuwa ni uchakavu na kupauka kwa vitambaa wanavyotumia sasa

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam  jana, Mratibu wa Kozi fupi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika banda la maonesho yanayoendelea  Viwanja Sabasaba, Mashaka Kasara, alisema hatua hiyo inatokana na malalamiko ya kuchakaa na kupauka kwa sare hizo.

Alisema katika kutekeleza mkakati hiyo, tayari wamefanya vikao kadhaa na wadu wengine, wakiwamo Chama cha Wamiliki wa Mabasi Dar es Salaam (DACOBOA), Umoja wa Wasafirishaji Abiria, Dar es Salaam (UWADAR) na kikosi cha usalama barabarani.

 “Kweli zile nguo zinachakaa, ni changamoto tutabadili kitambaa cha kushona kabisa,tulipendekeza kuwa na rangi damu ya mzee nyeusi (dark maroon) kwa mujibu wa wataalamu wa aina ya vitambaa,” alisema

Alisema VETA watahusika na kutengeneza sare hizo mpya ambazo kila dereva na kondakta wake atatakiwa kuwa nayo.

“Hizo za mara kwanza za rangi ya blue zimepauka na kuchoka hivyo ni vymea kuwabadilishia nao wakaonekana wasafi machoni mwa wateja wao. Na maamuzi haya hatujakaa VETA pekee iliundwa kamati ambayo mpaka ilipendekeza aina ya vvitambaana sehemu ambayo itapatikana vitambaa hivyo,” alisema

Katika hatua nyingine, Kasara alisema chuo hicho kinatoa kozi fupifupi ikiwemo ya ushonaji nguo, maabara, ufundi wa magari na udereva.

“Kwa mahitaji ya kujua namna ya kushona ,kukata nguo, rangi ubunifu wa mitindo kwa kutumia kompyuta, batiki na ufumaji wa masweta,soksi hivyo  chuo  kinawakaribisha watu kufika na kujifunza kozi hiyo kwa kuwa ni ajira tosha,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles