25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda kupambana na lishe, udumavu

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesaini mkataba na wakuu wa wilaya zote tano za mkoa huo  kuhakikisha suala la afya na ukuaji wa watoto.

Akizungumza katika hafla hiyo   Dar es Salaam jana,   Makonda alisema mkataba huo uliosainiwa ufanyiwe kazi  kupunguza asilimia 14.6 za watoto wenye udumavu sugu jijini.

Amewataka makatibu tawala katika wilaya zote kuhusisha suala la lishe katika vikao vyote vya manispaa hasa kwa Wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala ambazo zinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto ikilinganishwa na Ubungo na Kigamboni.

Aliwataka wananchi kuzingatia mlo kamili na usafi katika kuandaa mlo wa watoto kabla ya siku 1000 za mabadiliko kutoka kutokwa kutungwa kwa mimba hadi mtoto afikapo miaka miwili.

Mratibu Lishe kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waibe, alisema  hayo yote ni maelekezo ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha suala la lishe linapewa kipaumbele  watoto waweze kukua katika afya na akili.

“Kuanzia mimba inapotungwa hadi mtoto kufikia miaka miwili takribani siku 1000 ni siku pekee za kumtengeneza mtoto hasa katika ubongo kwa kuzingatia lishe, na baada ya hapo  mtoto hataweza kuepuka udumavu alioupata,” alisema Mwita

Aliitaja mikoa ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa chakula ndiyo inayoongoza kwa udumavu ikiongozwa na Rukwa yenye asilimia 50, Katavi, Ruvuma na Mbeya.

Naye Ofisa Lishe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mzamva, alisema hali ya lishe jijini  si nzuri   kwa vile  asilimia 34 katika utafiti uliofanyika 2014 unaonyesha watoto wana udumavu kwa kukosa lishe.

Alisema asilimia 3.7 ya watoto wana ukondefu, 20.2 wana uzito uliokithiri (obesity) asilimia 59  ya watoto chini ya miaka mitano wana upungufu wa damu na amewataka wakuu wa wilaya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mkataba huo.

Mikataba hiyo iliyosainiwa na wakuu wa wilaya ni agizo la taifa la kutenga Sh 1000 kwa kila mtoto chini ya miaka mitano, kupata matone ya vitamini A  na matibabu ya utapiamlo mkali kwa watoto chini ya miaka mitano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles