24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda atembelea waathirika wa mvua Dar

AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefanya ziara kukagua athari za mafuriko katika Wilaya ya Kinondoni.

Alisema  serikali imeanza kukarabati miundombinu iliyoathiriwa na mvua  inayoendelea kunyesha yakiwamo madaraja, barabara, mito na mifereji.

Akizungumza jana baada ya kutembelea nyumba zilizoathiriwa na mvua hiyo eneo la Jangwani, Makonda alisema miongoni mwa maeneo yanayoboreshwa ni eneo la Mto Msimbazi wenye urefu wa kilometa 19 na eneo la Jangwani ambalo maboresho yake yatagharimu zaidi ya Sh  bilioni 200 ikiwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Alisema   hadi sasa   watu wawili wamefariki dunia kutokana na mvua.

Pia aliwapa pole wananchi waliokumbwa na mafuriko wakiwamo wale ambao mali zao zimeharibiwa na wengine kulazimika kuyahama makazi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles