27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Makinda awafunda wabunge, madiwani viti maalumu

Mwandishi wetu -Mwanza

SPIKA mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, amewataka wabunge na madiwani wa viti maalumu kusimamia kikamilifu rasilimali za umma ili ziwanufaishe wananchi wote.

Hayo aliyasema juzi jijini Mwanza katika semina ya kujenga uwezo kwa viongozi wanawake wa Serikali za Mitaa (Wasemi) iliyoandaliwa na Shirika la TGNP Mtandao.

Alisema mchango wa wabunge na madiwani wa viti maalumu umekuwa hauonekani vizuri au kutambuliwa na jamii kutokana na wao wenyewe kuwa na hofu inayotokana na kutokujiamini kitu ambacho kimechangia kuwarudisha nyuma na kushindwa kuendelea mbele.

“Tatizo letu sisi viongozi wanawake tunajenga hofu, tunaogopa sana kujitokeza na kuwajibika vizuri kwa wananchi, eti kwa sababu ni viti maalumu.

“Sisi tulianzia pia viti maalumu, lakini tulipata nafasi ya kwenda jimboni kwa sababu tulijiamini, tuliwajibika kikamilifu na tulihakikisha uwezo wetu unaonekana na kila mmoja.

“Jitokeze kwa wananchi, watumikie kwa uadilifu na watakuona na kutambua mchango wako,” alisema.

Makinda aliwaasa wanawake viongozi wa Serikali za mitaa, kuhakikisha wanasimamia ubora wa huduma za jamii katika halmashauri zao na kuhakikisha kila kinachofanyika wanakielewa vizuri na kutoa taarifa kwa wananchi wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles