30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAKAMISHNA WAIKIMBIA TUME YA UCHAGUZI KENYA

NAIROBI, KENYA


MZOZO unaoendelea kushuhudiwa katika Tume Huru ya Uchaguzi na Uratibu wa Mipaka (IEBC) umeonekana kuchukua mkondo tofauti baada ya makamishna watatu kujiuzulu jana.

Katika taarifa ya pamoja, Naibu Mwenyekiti Consolata Nkatha-Maina, makamishna Paul Kurgat na Margaret Mwachanya wamemlaumu Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati wakisema ameshindwa kukiongoza chombo hicho na kuleta mshikamano unaotakiwa.

Taarifa hiyo iliyosomwa na Kamishna Mwachanya inasema kuna maswala mengi yaliyopaswa kushughulikiwa lakini Chebukati alipuuza kuyatatua.

Unapoona kiongozi kama mimi anachukua hatua ya kujiuzulu ujue kuna sababu maalumu, ambazo tumejaribu kueleza lakini hazijaangaziwa,” alisema Mwachanya katika mkutano na wanahabari jijini hapa.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa IEBC inaendelea kusambaratika chini ya Chebukati, ikionekana kugawanyika kwa misingi ya kisiasa na ubinafsi ba kwamba mwenyekiti huyo amekosa msimamo dhabiti.

“Tulipoingia ofisini, tuliapa kufanya kazi kwa uwazi na uaminifu haiwezekani kuwe na mvutano kati ya mwenyekiti na naibu mwenyekiti. Tume inaendelea kusambaratika huku maswala yetu ya ndani kwa ndani, hasa yale muhimu yakifichuka,” alisema Mwachanya kwenye taarifa hiyo.

Wiki iliyopita, Chebukati alimpa likizo ya lazima Ofisa Mtendaji Mkuu, Ezra Chiloba akimtuhumu kuhusika na matatizo yanayoikumba IEBC.

Afisa huyo aliwasilisha malalamiko yake mahakamani ili kumzuia kufukuzwa lakini mahakama iliyatupilia mbali.

Hatua hiyo ilisababisha migawanyiko zaidi, ambapo makamishna waliojiuzulu waliripotiwa kuegemea upande wa Chiloba huku Chebukati akiungwa mkono na makamishina Boya Molu na Profesa Abdi Guliye.

Mgawanyiko kama huo ulishuhudiwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8 mwaka uliopita pamoja na kabla ya marudio ya Oktoba 26, ambapo Kamishna Dk. Roselyn Akombe alijiuzulu kwa madai ya baadhi ya makamishna kuegemea mirengo ya kisiasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles