24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAKALLA AWAJIA JUU MAOFISA MADINI

NA PENDO FUNDISHA-MBEYA


MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, amewataka wataalamu wa Ofisi ya Madini kufanya utafiti wa kutosha wakati wa utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini ya dhahabu mkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema hayo jana, wakati akisikiliza kero za wananchi wa mkoa wake.

Makalla alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza kero, migogoro na malalamiko baina ya wachimbaji wadogo, wa kati na wale wakubwa.

Alisema, wataalamu wamekuwa wakifanya kazi kupitia mafaili ofisini na kujikuta wakitoa maamuzi yasiyo sahihi badala ya kutoka nje kwenda kujiridhisha katika maeneo husika, hivyo kuchangia kuibua kero na migogoro kwa wachimbaji wadogo na wawekezaji.

“Wachimbaji wadogo wanaitupia lawama ofisi ya madini, hasa katika suala nzima la utoaji wa leseni, wanasema wao wanafanya kazi kubwa ya kutafiti maeneo yenye madini, lakini maeneo hayo yamekuwa yakitolewa kwa watu wengine, tena wanaotoka nje ya eneo husika,” alisema.

Alisema, ofisi hiyo inapaswa kujiridhisha kwa kufika kwenye maeneo ya ardhi, hasa yale yanayoombwa na wachimbaji wadogo kwa ajili ya kuyakagua na kisha kutoa leseni, lengo likiwa ni kupunguza malalamiko.

Aidha, Makala aliahidi ofisi yake kuyafanyia kazi malalamiko yote yaliyotolewa na wananchi, wakiwamo wachimbaji wadogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles