24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Majipu 210 bandari

Tanzania's President elect Magufuli addresses members of the ruling CCM at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam*Makampuni yazuiwa kutoa huduma

*Yapo ya vigogo, wafanyabiashara wakubwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MOTO wa Rais Dk. John Magufuli umezidi kuwaka ndani ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambapo safari hii kibao kimegeuka kwa kampuni za mizigo 210 kuzuiwa kupitisha mizigo yao.

Uamuzi huo wa TPA umekuja miezi michache tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam na kubainika upotevu wa makontena zaidi ya 2000 kupitishwa bila kulipiwa kodi kwa mujibu wa sheria.

Taarifa iliyotolewa jana na kusainiwa na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Fred Liundi, ilieleza kuwa uamuzi huo umechukuliwa kwa sababu ya kushindwa kuwasilisha vielelezo vya malipo, kama walivyotakiwa na TPA.

Pia wameshindwa kufika bandarini kupokea nyaraka kadhaa kuhusu madeni wanayodaiwa na TPA kwa mujibu wa mizigo yao waliyopitisha.

“Makampuni yafuatayo ya kupitisha mizigo bandarini (Clearing and Forwarding Agents) yamezuiwa kufanya kazi katika bandari zote zinazomilikiwa na TPA pamoja na washirika wake (ICS’s, CF’s na TICTS) tangu Februari 9, mwaka huu. Uamuzi huo umechukuliwa kwa sababu ya kushindwa kuwasilisha vielelezo vya malipo, kama walivyotakiwa,” alisema Liundi katika taarifa yake.

Akizungumzia uamuzi huo, Meneja Mawasiliano wa Bandari, Janeth Luzangi, alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kampuni hizo kushindwa kuwasilisha uthibitisho wa malipo ya mizigo yao kwa TPA.

“Tulitoa muda kwa makampuni haya na kuwataka kuwasilisha vielelezo vya malipo ya mizigo yao, lakini hawakufanya hivyo, sasa tumelazimika kusitisha utoaji huduma kwao hadi pale watakapowasilisha na si vinginevyo,” alisema Luzangi.

 

UKIMYA WA TAFFA

Kutokana na uamuzi huo wa Bandari, MTANZANIA ilimtafuta Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Steven Ngutunga, ili kupata msimamo wao lakini simu yake haikupatikana.

Lakini taarifa kutoka kwa baadhi ya wamiliki wa makampuni hayo, zinadai kuwa baadhi yao walikamilisha utaratibu uliotangazwa na TPA.

“Sisi tulitimiza masharti yote ikiwamo kulipa malimbikizo ya madeni, sasa sijui hili linatoka wapi. Kuna kila dalili kwa bandari kukosea orodha na kutaja kampuni yetu,” alisema mmoja wa wakurugenzi wa moja ya kampuni zilizozuiwa kutoa huduma.

 

ORODHA YA MAKAMPUNI

Kampuni zilizozuiwa kutoa huduma bandarini ni 21st Century Freight Forwarders, Aristepro Investment Co. Ltd, Ace Exim, Ally Vay C & F Agency, A & D Holdings Ltd, A & G Holdings Ltd, ACW Investment Ltd, Afro Centre (T) Ltd, Allmol Trading, Amico Trading Ltd, Avow Holding (T) Ltd, Afritel Systems Ltd, Afrovision International Co. Ltd, Arusha Cargo Clearing & Forwarding Ltd.

Nyingine ni Arusha Freight Transport Agency, Bakhresa Food Products Ltd, Boston Forwarders Ltd, Babylon Freight Ltd, Beam Tanzania Ltd, Best Ocean Air Ltd, Break Through Holdings Ltd, Business Service Promotion Ltd, B & J Co. Ltd, BNM Co. Ltd, Boneste General Enterprises Ltd, Blue Light Investment Ltd, BN Metro (E.A) Ltd, Cad Mulungu Co. Ltd, Capital Cargo Removers Ltd, Cargo Stars Ltd.

Kampuni nyingine ni Car Freight Station ICDV, Clear Services Tanzania Ltd, Clampek (T) Ltd, Classic Choices Investment Ltd, Continental Reliable Clearing Ltd, Conanza Express Ltd, Cos Africa Logistics Ltd, Cosmos Haulage Co. Ltd, Chissel C & F Ltd, Cusna Investment Ltd na Daffor Enterprises Ltd.

Katika orodha hiyo pia wamo Dynamic Freight Forwarders Ltd, Datar & Co. Ltd, Dar es Salaam Global Access Ltd, Dar Coast Enterprises Ltd, Denilo Freight Ltd, Destination Tanzania Cargo Logistics, Divine Cargo Services Ltd, Dow Elef Ltd, Dolusi (T) Ltd, Dolphin Sea And Air Ltd, E-3 Freight Co. Ltd, Eagle Tallons (T) Ltd, Econ Consult & Trading Co. Ltd, Eltex Investment Ltd, Edams Holdings Ltd, Efficient Freighters (T) Ltd, Equity Agencies na Expro Freight Services Ltd.

Wengine ni Evergreen General Logistics (T) Ltd, Enterprises Logistics Ltd, East African Fossils Fossils Ltd, Fedrol Cargo Ltd, Full Cargo Support Ltd, Freight 24/7 Ltd, Favre Freight Forwarders Ltd, Freight Forwarders (T) Ltd, Freedom Freight Forwarders Ltd, Fifa & Flow Co. Ltd, F.K. Farms & Co. Ltd, First Choice Clearing & Forwarding Ltd, Freight Works Ltd, Frafza Freight Forwarders Ltd, General Envirocare (T) Ltd, General Shami Investment Co. Ltd na Glory Freight Ltd.

Pia zipo kampuni za Grand Movers Co. Ltd, Gwiholoto Impex Ltd, GS InterTrade Co. Ltd, Hamymack Trading Co. Ltd, Hadolin (T) Ltd, Hasa Customs Agency (T) Ltd, Horizon Freight Forwarders Ltd, Hodari Freight Ltd, Hardmark Logistics Ltd, HK Freight Forwarders Ltd, Hotreef Trading Ltd, Home Base Tanzania Ltd, Ilemela Investment Ltd, Impact Trading And Investment Co. Ltd, Jambo Freight Ltd, Jas Express Ltd, Jamaap Co. Ltd, Joe Ocean C & F Ltd, Juhudi Clearing And Forwarding, Juni Trust Freight Tz Ltd.

Mbali na hizo zipo pia kampuni za Kas Freight Ltd, Kahe International Ltd, Kassam Freight Ltd, Kiwaepa International Co. Ltd, Khan’s C & F Ltd, Kams Trading Ltd, Kings Freight (T) Ltd, K & K Cargo Logistics, K&K Company Ltd, Kadengere Traders Ltd, Korufreight (T) Ltd, Lawia (T) Ltd, Laz Ltd, Lesidi General Cargo Ltd, Liberal International Ltd, LCR Limited, LDV Macro Investment Ltd na Logistics Efficiency Co. Ltd.

Pia zipo kampuni za Lesheti Trading Ltd, Lichinga (T) Ltd, Mambona Freight Ltd, Mamba Enterprises Ltd, Maxima C & F Ltd, Mwaya C & F, Marine Air Freight Ltd, Maritime Shipping Consultants, Mechanised Cargo Systems, METL, Metrologic C &f F Ltd, Minex Logistics Ltd, Mpepa Traders Co. Ltd, Mogo Forwarders Ltd, Mokha Agency Co. Ltd, Mwagy Investment Ltd, Naito General Supplies Ltd, Nal Business Co. Ltd, Nemarts Limited na Neighbour Trading Co. Ltd.

Katika orodha hiyo TPA pia imeyazuia makampuni ya Ngaramau Contractors Ltd, Nutricare (T) Ltd, Nkira Trading Ltd, NM Freight Ltd, Overseas Hi-Tech Industrial Ltd, Orbit Freight Ltd, Pasiwa Cargo Ltd, P & D Freight Forwarders Ltd, Platinum Trading Co. Ltd, Palm Swift Tz Ltd, Quality Logistics Ltd, Runner Co. Ltd, Rungwe Trading Ltd, Reindeer Investment Ltd, Regent (T) Ltd na Rukwi Holdings Ltd.

Kampuni nyingine ni Royal Freight Ltd, Ruma International Ltd, R.H.G General Traders Ltd, Sky Land Across Freight, Sai C & F Ltd, Shift Cargo Ltd, Sachsen Spedition Ltd, Sahara Desert Freighters, Sahuse Services & Supplies Ltd, Selwek & Solar Forwarders Ltd, Sami Agency Ltd, Sahe C & F Ltd, Sangare Express Ltd, Sea Bridge Co. Ltd, Sea Air Forwarders Ltd, Sea Africa Cargo Freight Ltd, Scol (T) Ltd, Shakura Trading Services, Space Land Logistics, Senkondos Import & Export Ltd, Smith Freight Forwarders Ltd, Sino Logistics Ltd, Scanland Shipping Consultants Ltd, Spaceland Logistics Ltd, Sachsen Spedition Ltd, Swiftways International Ltd na Stepio Freight Ltd.

Nyingine ni Switch Trade Ltd, Sun Fresh Co. Ltd, Star Vision International Ltd, Tanga Cargo & Trust Ltd, Trade Waves Investment Co. Ltd, Transit Ltd, Trident Clearing Ltd, Team Freight, Trans Net Freighters, Three Way Shipping Service Ltd, Trans Pack Tanzania Ltd, Trans African Forwarders Ltd, Trans Barriers Freight Ltd, Transit Ltd, Tripple D, Twende Freight Forwarders Ltd, Ujiji C & F Ltd, United Youth Shipping Co. Ltd, United Family Co. Ltd, Uwanji General Traders Ltd, Uprising C & F Ltd na Upland Freight Ltd.

Fukuzafukuza hiyo ya bandari pia imeyagusa makampuni ya Vigu Trading Ltd, Vamwe Investment Co. Ltd, Viccom Resources Co. Ltd, Way Logistics Ltd, West Freight Forwarders, Wings Wheels Co. Ltd, Walmax Freight Forwarders Co. Ltd, Xpress Maritime Agency Co. Ltd, Zappex International Ltd, Zaihuse C & F Ltd na Zzoikos (T) Ltd.

 

WATUMISHI WASIMAMISHWA

Desemba 29, mwaka jana TPA iliwakamata watumishi wake 15 ambao wanadaiwa kuhusika na ukusanyaji wa malipo ya tozo ‘Wharfage’ na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 47.418 kwa kutoa makontena 11,884 kwenye bandari kavu (ICD) saba.

Pamoja na hatua hiyo, ulianza msako wa kuwatia mbaroni mawakala ambao bado hawajalipa kodi, ambapo kufikia Januari 10, mwaka huu walitakiwa wawe wamefikishwa polisi ili waweze kulipa fedha wanazodaiwa kwa mujibu wa sheria.

Watumishi hao 15 pia wanadaiwa kuisababishia hasara Serikali ya Sh bilioni 1.072 za malipo ya tozo ‘Wharfage’ kwa magari 2,019 katika CFS sita.

Baada ya kubaini hali hiyo, Desemba 28, mwaka jana TPA iliwafikisha polisi watumishi hao ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Watumishi hao ambao wametajwa katika taarifa hiyo ni Nathan Edward,  John Elisante, Aron Lusingu, Aman Kazumari, John Mushi, Valentino Sangawe, Leticia Massawe, Christina Temu, Merina Chawala, Happygod Naftai, Adnan Ally, Masoud Seleiman, Bonasweet Kinaima, Benadeta Sangawe na Zainab Bwijo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles