Imechapishwa: Fri, Jul 8th, 2016

Majambazi yavamia kijiji Kagera

SMG

NA EDITHA KARLO, Bukoba

MAJAMBAZI ambao idadi yao haikujulikana, wamevamia Kijiji cha Benaco katika Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Abel Mtagwa, alisema jana kuwa majambazi hao walivamia kijiji hicho juzi usiku na kupora Sh milioni 2.4 kutoka kwa mfanyabiashara mmoja kijijini hapo.

Alisema     mfanyabiashara aliyeporwa fedha hizo anajishughulisha na miala ya simu ya M-pesa.

“Wakati wa tukio hilo, majambazi hao walikuwa na bunduki moja  ya SMG na mabomu ya kurusha kwa mkono.

“Lakini  wakati majambazi hao wanajiandaa kuondoka eneo la tukio, walimjeruhi kwa risasi mwanafunzi mmoja anayesoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Gankabo iliyoko Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.

Mwanafunzi huyo,   Nelson  Simon (15) kwa sasa amelazwa katika Hospitali Teule ya Wilaya hiyo ya Murgwanza.

“Kwa hiyo, baada ya majambazi hao kufanya uhalifu huo walikimbia na kutokomea kusikojulikana, lakini  askari wameelekea eneo la tukio na msako mkali unaendelea katika maeneo yote ya mipaka katika wilaya hiyo,” alisema.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

FACEBOOK

YOUTUBE

Translate »

Majambazi yavamia kijiji Kagera