27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MAJAMBAZI WATATU WAUAWA DAR

Mmoja wa majambazi aliyeuwawa wakati wa tukio la ujambazi lilitokea jana katika eneo la Mikocheni Dar es Salaam.
Mmoja wa majambazi aliyeuwawa wakati wa tukio la ujambazi Mikocheni, Dar es Salaam

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

WATU watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Mikocheni, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea jana mchana Mikocheni karibu na Shule ya Sekondari ya Wavulana Feza.

Ilielezwa kuwa majambazi hao walikuwa wakijaribu kuiba katika ofisi za Mkekabet zilizopo jengo la Milvik.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mmoja wa watuhumiwa hao wa ujambazi ni mwanamke aliyekuwa dereva wa gari walilotumia ambaye alifanikiwa kutoroka.

MTANZANIA ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Suzan Kaganda, alikiri kutokea tukio hilo.

“Nathibitisha kutokea kwa tukio hilo japo ni mapema sana kulizungumzia. Ninachoweza kusema ni kwamba tumefanikiwa kuzima jaribio la ujambazi na majambazi wawili wamekimbia, tunaendelea kuwatafuta,” alisema Kamanda Kaganda.

Matukio ya ujambazi Dar es Salaam yanaonekana kuanza kurejea kwa kasi.

Juzi watu wanaodaiwa kuwa majambazi walipora kiasi cha fedha zinazokadiriwa kuwa zaidi ya Sh milioni 25 katika gari lililokuwa makutano ya Barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara kwenye taa za kuongoza magari.

Tukio hilo lilitokea saa 4 asubuhi wakati gari hilo likiwa kwenye foleni ya magari eneo hilo.

Watu hao wameporwa katika eneo ambalo huwa askari doria wametanda, lakini wakikamata pikipiki zinazopita kutoka maeneo mbalimbali.

Taa za Tazara zilizoko makutano ya barabara kutokea Buguruni, Temeke, Kariakoo/Posta na Gongo la Mboto ndilo eneo lenye askari wengi wakiwamo wa usalama barabarani.

Wakati tukio likifanyika kulikuwapo askari wenye magwanda maalumu ya askari doria zaidi ya watano wakihangaika na waendesha pikipiki upande wa Barabara ya Mandela kutokea Buguruni.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa watu hao waliokuwa wakipeleka fedha hizo benki, hawakuwa na ulinzi kama inavyoshauriwa na Jeshi la Polisi.

Majambazi hao waliokuwa watatu, walipora fedha hizo katika gari dogo aina ya Toyota Rav4 lenye namba za usajili T 455 DFN mali ya kampuni ya kutengeneza mabati ya Sun Share lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyejitambulisha kwa jina la Richard Charles.

Kwenye gari pia alikuwapo mfanyakazi mwingine wa kampuni hiyo, mwenye asili ya China, aliyetambulika kwa jina la Cheng Deng.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles