24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Watanzania changamkieni fursa za biashara maonesho ya SADC

Anna Potinus, Dar es Salaam

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kutumia fursa ya maoneho ya nne ya wiki ya viwanda Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kujenga urafiki na wafanyabiashara wa mataifa hayo ya kigeni ili waweze kuja kuwekeza nchini.

Ametoa rai hiyo leo Jumanne Agosti 6, alipotembelea maonesho ya nne ya wiki ya viwanda Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Watanzania wanapaswa kutumia fursa hii kutanua wigo wa biashara kimataifa.

“Tunayo fursa ya kuhimiza mataifa ya nje kuja kuzalisha hapa kwetu kuungana na Watanzania wenye ardhi na mtaji ambao wanaweza kuunganisha na mtaji wa wageni wakaanzisha viwanda na kutanua wigo,” amesema.

“Wito wetu kwa Watanzania wenye uwezo wa kutumia nafasi hii kuunganisha nguvu na marafiki zetu kutoka nchi za SADC huu ndio wakati muafaka wa kuja kutambua nani anaweza kuja kuwekeza hapa kwetu ili tuweze kuunganisha nguvu na kutengeneza kiwanda kikubwa na kuweza kuzalisha bidhaa na mwenzako ataweza kutafuta masoko kwenye nchi ambazo amezifikia na nchi amabazo wewe pia umetafuta masoko, tukiziunganisha tunaona kabisa fursa ya kuweza kupata masoko ya bidhaa zetu,” amesema.

Aidha amesema maandalizi yote ya shughuli hiyo yamekamilika kwa kiasi kikubwa na tayari wameshapata ratiba ya uingiaji wa wageni, ambapo amewasishi Watanzania kutumia nafasi hiyo kuwaonesha heshima na ukarimu wageni wanaokuja nchini ili warudi katika mataifa yao wakiwa na ujumbe maalum.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles