27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Viongozi CCM zingatieni katiba ya chama

MWANDISHI WETU-BUKOBA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba ya chama   kuepusha migogoro kwenye maeneo yao.

Amesema chama chochote ambacho viongozi wake hawazingatii katiba lazima kiwe na migogoro kwa sababu  uzingatiaji wa katiba ni miongoni mwa mambo yanayokitofautisha Chama Cha Mapinduzi na vyama vingine vya siasa nchini.

Alitoa agizo hilo juzi alipozungumza na viongozi wa CCM, wabunge   na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kagera, alisema ni muhimu kwa viongozi hao kusoma na kuizingatia katiba ya chama kwa sababu inaelekeza misingi yote ya utendaji.

Aliwasisitiza wanachama na wapenzi wa CCM wasome katiba ya chama na kuzielewa kanuni, taratibu na sera  waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Akisisitiza jambo hilo, Majaliwa aligawa nakala za katiba ya hiyo kwa viongozi hao na kuwataka wazifikishe hadi kwenye ngazi ya mashina.

Kadhalika, alisema utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa nchi nzima unaendelea vizuri na kuhusu changamoto zilizopo katika baadhi ya maeneo nchini wanaendelea kuzirekebisha.

“Lengo lao ni kuhakikisha wanatekeleza ilani kama CCM ilivyoelekeza na ili kujiridhisha kama wanafanya vizuri lazima viongozi wawasimamie watendaji katika maeneo yao na watakapobaini kasoro wasisite kutoa taarifa.

“Viongozi chama lazima wajiridhishe kama huduma za maji, elimu, miundombinu ya barabara, kilimo pamoja nishati ya umeme zinapatikana kwenye maeneo yao yote na ni kwa kiasi gani,” alisema Majaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles