27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Tutumie mwezi wa Ramadhani kudumisha amani

Elizabeth Joachim, Dar es Salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania watumie mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kudumisha amani, mshikamano na kuwaombea viongozi wa kitaifa.

Katika taarifa iliyototewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo Mei 25 Dodoma, imeeleza kwamba Majaliwa amesema hayo jana aliposhiriki hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya NMB iliyofanyika mjini hapo.

‘’Mwezi huu tuna majukumu makubwa ya kufanya ibada, kutubu dhambi zetu, kuomba rehma kwa Mwenyezi Mungu, kudumisha mshikamano na kuwa wavumilivu na kila mwananchi aendelee kuliombea Taifa lizidi kudumisha amani na mshikamano.

Aidha Majaliwa ameipongeza benki ya NMB kwa huduma bora wanazozitoa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwa na matawi hadi vijijini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa benki ya NMB, Albert Jonkergou, amesema lengo la kuandaa hafla hiyo ya futari ni kuimarisha ushirikiano uliopo baina yao na wateja wao huku akiwataka Waislam katika kipindi hiki cha mfungo kumrudia Muumba wao na kumshukuru kwa mema yote anayowajalia waja wake.

“Mwezi wa Ramadhan ni kipindi muafaka cha kufuturu pamoja hivyo, nawashukuru wateja wetu kwa kujumuika nasi nawaomba muendelee kutumia huduma zetu.

Hafla hiyo ilihudhuliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson, Mashekhe wa Mikoa ya Kanda ya Kati (Dodoma, Singida na Manyara).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles