31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Tunaithamini sekta binafsi

Na Mwandishi Wetu -Dar es Salaam


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inathamini uwapo wa sekta binafsi nchini na inashirikiana nayo kuboresha maendeleo ya taifa.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana alipokutana na bodi mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ilipokwenda kujitambulisha.

Pia aliwapongeza Mwenyekiti mpya wa TPSF, Salum Shamte na wajumbe wa bodi hiyo kwa kuchaguliwa kuingoza taasisi hiyo.

“Serikali ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na taasisi hii kwa sababu ndiyo mwezeshaji wa kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025,” alisema.

Kwa upande wake, Shamte alisema sekta binafsi inatambua juhudi za Serikali za kuboresha mazingira ya biashara.

“Sisi tupo tayari kushirikiana na Serikali kwa kuwabana wafanyabiashara wanaoenda kinyume na maadili na sheria, ila tunaiomba ishirikiane nasi katika utekelezaji wake,” alisema.

Aliiomba Serikali iendelee kutoa vivutio kwa biashara zinazoanza ili kuhamasisha uwekezaji kwa kuwa baadhi yake zimeonesha gharama kubwa za uzalishaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles