31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Simamieni elimu kwa watoto wa kike

Mwandishi Wetu-Pemba

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya nchini wasimamie ipasavyo suala la elimu, hususani kwa watoto wa kike na kuchukua hatua kwa watakaowakatisha masomo.

Pia Majaliwa amesema Serikali inawataka  watoto watoe taarifa za watu wanaotaka kuwakatisha masomo yao kwa viongozi wa shehiya waliopo katika maeneo yao.

Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Daya kilichopo Mtambwe, Wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba.

Majaliwa alisema Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike, lengo likiwa ni kuhakikisha wanamaliza masomo yao na hatimaye waweze kujikwamua wao pamoja na familia zao.

Alisema watoto wa kike wanatakiwa waheshimiwe na jamii kwa kuachwa waendelee na masomo yao bila ya usumbufu wowote na atakayebainika kukatisha masomo adhabu yake ni miaka 30 jela.

“Wanafunzi wa kike hakikisha mtu yeyote atakayekugusa, kukufuatilia nenda kamshtaki kwa kiongozi wa shehiya husika. Vijana jihadharini na watoto wa shule, ukikutwa naye jela miaka 30,” alisema Majaliwa.

Awali, akisoma taarifa za ujenzi wa chuo hicho, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Madina Abdallah,  alisema hadi kukamilika, mradi huo utagharimu Dola za Marekani milioni 25.8, ambazo kati yake dola milioni 23.4 zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) huku dola milioni 2.4 zikitolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Alisema kwa mujibu wa mkataba wa mradi huo kazi ya ujenzi inajumuisha vituo viwili vya mafunzo ya amali ambavyo ni Makunduchi, Unguja na Daya, Pemba. Pia upanuzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Utalii Maruhubi na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufundishia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles